JUMLA ya timu 30 za mchezo wa darts zinatarajia kuchuana leo katika mashindano ya taifa ya mchezo huo yanayotarajia kufanyika katika ukumbi wa Rose Garden uliopo Area C, Dodoma.
Timu hizo ni kutoka katika mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Temeke, Mbeya, Ilala na Kinondoni ambapo mshindi atapata vikombe na pesa taslimu ikiwa ni pamoja na zawadi mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Darts Tanzania, Gesase Waigama alisem
a mashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa Mkoa kwa Mkoa na baadae yatachezwa kwa mchezaji mmoja mmoja ikiwa ni kwa mtindo wa ligi.
Alisema, timu zote zimeisha wasili Morogoro ambapo maandalizi yote ya kufanyika kwa mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya TBL kwa kupitia kinywaji chake cha Safari lager.
"TBL wametupa ufadhili mkubwa na tunawashuru kwa kutuwezesha kutupa udhamini huo ili kufanikisha mashindano haya kwa lengo la kukuza mchezo huu ambao baadae utakuja kuliletea sifa Taifa kwa kutwaa ubingwa wa Kimataifa," alisema Waigama.
Naye kwa upande wake Meneja wa Safari lager Oscar Shelukindo alisema, wamedhamini mahitaji yote kwa timu ikiwa ni pamoja na zawadi zitakazotolewa katika mashindano hayo.
Alisema, lengo hasa la kudhamini mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unakuwa miongoni mwa michezo mikubwa nchini ambao takuja kutoa timu bora ya Taifa itakayowakilisha katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment