PROMOTA wa pamabano kati ya Francis Cheka na Karama Nyilawila Philemon Kiyando 'Don King' amesema yuko tayari kuwaburuza mahakamani Shirikisho la masumbwi Tanzania (PST) kama litasitisha pambano hilo.
sambamba na kuwaburuza mahakamani pia ataomba shirikisho hilo lifungiwe kutokana na kutomtendea haki kwa kumtaka Nyilawila kutokucheza pambano hilo ikiwa tayari ameishatumia gharama nyingi kuliandaa hadi sasa na kutaka kulisitisha wakati siku zimekaribia.
pambano hilo limepangwa kufanyika Januari 28 katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro likiwa katika uzito wa kg 72 raundi 12 lisilo la ubingwa.
Wakati mabondia wakiendelea kujifua Rais wa PST Emmanuel Mlundwa alitangaza pambano hilo kutokuwepo kutokana na Nyilawila kutakiwa kutetea ubingwa wake wa WBF nchini Ujeruman Februari 11 dhidi ya Mjeruman Erims Cagri.
Akizungumza na Majira Promota huyo alisema ameishatumia pesa nyingi sana kuandaa pambano hilo na tayari ameishalipia uwanja huo kwa ajili ya pambano itakuwaje liahirishwe bila kufahamishwa mapema kabla ajatumia gharama zote.
"Nimelipa mabondia, uwanja na nimeishafanya maandalizi makubwa sasa itakuwaje niahirishwiwe pambano hilo na nani tanilipa gharama zangu? mimi siwaelewi nanipotayari kuwapeleka mahakamani kwakunitia hasara kiasi kikubwa na wala sitahirisha pambano," alisema Kyando.
Alisema, kama wataweza waahirishe pamabano lao lakini pambano lake lipo palepale kama wataweza wamrudishie gharama zake zote alizotumia.
Alisema, wakati wote anaandaa pambano hilo ajapewa taarifa yoyote na PST hata kwa maandishi yeye amekuwa tu akiona kwa vyombo vya habari sasa kama ni msimamizi mzuri kwanini asimwite au amtumie barua ili asitishe maandalizi hayo.
Promota huyo alisema, yeye kama mdau wa michezo asingeweza kung'ang'ania Nyilawila acheze pmabano hilo kama tayari anapambano la kutetea ubingwa lakini bondia huyo alimfata na kumtaka amuandalie pambano kutokana na kukaa muda mrefu bila kupanda ulingoni kitu ambacho sio kizuri kwa mabondia.
"Nyilawila alikaa miezi 18 bila kupanda ulingoni na akaamua kuniomba nimuandalie nikaamua kumuandalia sasa iwaje gharama zote za maandalizi zitoke kwangu alafu ndio akatetee ubingwa huo mimi sikubali hata kidogo wao walikuwa wakimzungusha kumuandalia nimetumia gharama ndio wapitie mgongo uwo haiwezekani," alisema Kyando.
Kukaa muda mrefu kunamchangia kumshusha kiwango bondia na hasa ukizingantia anaenda kutetea ubingwa si atapigwa sana kwani hana mazoezi na mazoezi ya ndani tu hayamsaidii.
Alisema, pambano hilo pia lingemsaidia Nyilawila kufanya vyema kwani kama amekaa muda mrefu bila kupanda ulingoni hivyo angeweza kukutana na Cheka ingemsaidia kumpastamina na hata kuweza kutetea vyema mkanda wake huo.
Alisema, PST hawana utaratibu mzuri kwani wanawakandamiza mapromota wa Tanzania na hiyo inachangiwa na wivu na chuki badala ya kushirikiana na mapromota kwa ajili ya kukuza michezo kwa ajili ya kuwainua mabondia wa hapa nchini kwani hata mapambano ya nje wanayoenda kupigania wanalipwa kiasi kidogo cha fedha tofauti na hapa nyumbani.
"Hapa kunafitina fukani kwani hata mwaka 2006 ilishawahi kunitokea nikaamua kukaa kimya na kuacha kuandaa mapambano lakini Nyilawila alivyoniomba nikaamua kurudi tena," alisema.
Lakini kwa upande wa Nyilawila amedai hatoweza kupanda ulingoni kucheza pambano hilo na Cheka kama alivyoamriwa na PST ambao ndio wanamsimamia katika pambano lake hilo la nje.
No comments:
Post a Comment