BENKI Kuu ya Tanzania(BOT) imetakiwa kujiridhisha kuwa benki zilizopo nchini zinafanya biashara halali na siyo na kutunza fedha haramu.
Hayo yamebanishwa jana jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu hazina,Bw. Laston Msongole wakati wa semina ya kuwapatia ufahamu wa athari zitokanazo na biashara ya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi ambayo huathiri uchumi wan chi husika.
Bw.Msongole alisema kuwa vyombo vya dola vikiwemo polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa PCCB pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania TRA vimepewa changamoto nyingi katika mapambano dhidi ya biashara hiyo haramu.
Alisema kuwa biashara hiyo mbali na kuathiri uchumi wa taifa pia imekuwa ikisababisha kushamili kwa wimbi la uhalifu si Tanzania tu bali ni kwa dunia nzima.
Aliongeza kuwa, shughuli hizo ni za jinai na hazina tija kwa nchi yoyote kwa kuwa ni changamoto hivyo nguvu ya pamoja inahitajika ili kufanikisha vita hiyo.
Shughuli hizo haramu ambazo hufanyika nje ya mkondo halali wa mzunguko wa kifedha kutokana na wahusika kuhofia kubainika maovu yao.
"Miongoni mwa shughuli zinazopelekea kuwepo kwa fedha haramu ni pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya, uuzaji wa silaha, rushwa na shughuli za ujambazi"alisema Bw.Msongole
"Unajuwa hii biashara ya fedha haramu imekuwa ikichangia kuporomoka kwa utawala bora na sheria, kuyumba kwa sekta ya fedha ambayo hupelekea uchumi kuporomoka, kuporomoka ushindani na kufukuza wawekezaji"aliongeza
Pia alisema kuwa michezo ya kamali ambayo huchezwa kwenye club za usiku hutumika kama njia halali ya kupitishia fedha chafu kwenye mzunguko halali wa kifedha.
"Watanzania muwe mnatoa taarifa kwa vyombo vya dola na mamlaka husika pindi mnawapobaini watu mwenye utajiri mkubwa tofauti na vipato vyao ili uchunguzi ufanyike kwa ajili ya kubaini chanzo cha mapato vyao"alisisitiza
Biashara ya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi,ilianza miaka mingi lakini mwaka 2001 mara baada ya majengo ya biashara ya Marekani (WTO) kushambuliwa na magaidi wa kikundi cha Al-Qaida,nchi mbalimbali zilioanza kuitumia sheria ya kupinga biashara hiyo ambapo Tanzania ilianza rasmi kuitumia mwaka 2006 baada ya kuundwa kwa kitengo cha kushughulikia biashara hiyo kilichopo ndani ya Wizara ya Fedha.
No comments:
Post a Comment