24 January 2012

Mshambuliaji Burkina Faso ahangaika kujiweka sawa

LIBREVILLE, Gabon

KOCHA wa Burkina Faso, Paulo Duarte amesema kuwa mshambuliaji, Alain Traore anahangaika kujiweka fiti kwa ajili ya michuno ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 iliyoanza Jumamosi.

Mchezaji huyo mwenye miaka 23 anakipiga katika timu ya Auxerre, ni muhimu katika timu yake ya taifa na kocha wake amekuwa na mashaka juu ya kukosekana kwake.

"Alain Traore amekuwa akipambana na umajeruhi ambao umemweka nje ya uwanja kwa zaidi ya siku nne. Bahati mbaya kwa kuwa hii imeathiri uchezaji wake alisema," Duarte wakati akizungumza na Sidwaya.

"Ninatumini anarejea na kuwa fiti haraka na si kuwa katika asilimia 50 hadi 60. Kitu cha muhimu zaidi kwake ni kuendelea na mazoezi."

Burkina Faso iko katika Kundi B sambamba na Sudan, Angola na Ivory Coast ambayo inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa. Burkina Faso ilifungwa mabao 2-1 katika mechi yake ya kwanza dhidi Angola mjini Malabo.

Traore ndiye alifunga bao pekee la Burkina Faso baada ya kuchezeshwa akiwa hajawa fiti kabisa.

No comments:

Post a Comment