24 January 2012

Kocha Zambia ajiamini kuifunga Senegal

MALABO, Equatorial Guinea

KOCHA wa Zambia, Herve Renard ameanza kujiamini baada ya kuona timu yake ya Zambia ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi.


Zambia ilifunga mabao mawili ya kuongoza katika mechi ambayo yaliwekwa kimiani na Emanuel Mayuka na Rainford Kalaba katika kipindi cha kwanza.

Senegal ilirudisha bao moja kupitia kwa Dame N'Doye, lakini hakuweza kubadilisha matokeo kwani mechi iliisha kwa Zambia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Renard alisema Zambia ilivuruga mipango ya wapinzani wao.


"Sisi tulijua fursa ya kufunga ilikuwa kucheza nyuma ya mabeki wao, kwa sababu wana nguvu sana katika mipira ya juu," Renard alisema.

"Sisi tulifanya hivyo kwa ukamilifu katika nusu ya kwanza."

Alipoulizwa juu ya matokeo kuwashangaza watu wengi, Renard alisema upande wake ulikuwa na ujasiri wa kwenda katika mechi dhidi ya moja ya timu zinazopewa nafasi kutwaa ubingwa katika mashindano hayo.

"Haikutushangaza. Ni matokeo yaliyotokana na kufanya kazi ngumu. Sisi tulijua tulikuwa na uwezo wa kufanya hivyo," alisema.

Zambia katika mechi yao ijayo ya Kundi A itacheza na Libya kesho.

No comments:

Post a Comment