24 January 2012

Kocha Sudan adai wasiwasi uliwaponza

LIBREVILLE, Gabon

KOCHA wa Sudan, Mohamed Abdalla ametaja sababu kubwa iliyochangia timu yake kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast ni kucheza kwa wasiwasi dhidi ya wapinzani wao.

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal, Ivory Coast ambayo inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa AFCON, waliwafunga Sudan bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Malabo ambapo bao liliwekwa kimiani na Didier Drogba dakika ya 39 kwa kichwa.


"Kucheza na timu kama ya Ivory Coast ikiwa na nyota wake wote na ikiwa inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa katika fainali, tulikuwa na wasiwasi.

Abdalla alisema kuwa kwa sasa timu yake inawaza kuhusu mechi ijayo dhidi ya Angola ambayo itachezwa Alhamisi.

"Ninainoa timu ambayo inawachezaji vijana na wasio na uzoefu. Sijasikitishwa na uchezaji wa wachezaji. Lakini haina maana kuwa nimeridhishwa na matokeo. Tutarejea kazini kwa ajili ya mechi ijayo.”

Kuutokana na Angola kushinda bao 2-1 dhidi ya Burkina Faso, Sudan imejikuta ikiwa na mwisho kwenye Kundi B ikiwa haina pointi sawa na The Stallions, wakati Ivory Coasti ikiwa na pointi tatu sawa na Angola.

No comments:

Post a Comment