24 January 2012

Equatorial Guinea waitia nguvu Gabon

LIBREVILLE, Gabon

USHINDI ilioupata Equatorial Guinea dhidi ya Libya umewatia matumaini wenyeji wenzao Gabon katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012.

Kumekuwa na usemi kuwa "kama Equatorial Guinea imeweza, sisi wa wa-Gabon tunaweza pia”, wakimaanisha ushindi wa Nzalang wa bao 1-0  dhidi ya  Libya katika Uwanja wa Bata Jumamosi ambapo Gabon ilianza mechi yake ya kwanza dhidi ya Niger mjini Libreville.

Kutokana na nchi hizo kuwa karibu  na utamaduni wao kufanana wa- Gabon walikuwa wakiishangilia Equatorial Guinea dhidi ya mahasimu wao kutoka Kaskazini.

Equatorial Guinea maarufu kama Nzalang Nacional, imekuwa na mshikanano na kucheza soka ya kufurahisha, ilishinda bao 1-0 na kufanya mashabiki wa Gabon kufurahi kwa kushangilia.

Ushindi huo ulikuwa ukiwapa matumaini kuwa wao pia wanaweza kufanya vizuri katika mechi yao ya jana dhidi ya  Niger katika Uwanja wa d’Amitie mjini Libreville.

Gabon wanashiriki mashindano ya Afrika kwa mara ya tano ikiwa ni timu ya Ukanda wa Afrika ya Kati ambao timu kama Cameroon na Kongo zimekuwa zikitawala.

Coach Gernot Rohr aliwataka wachezaji wake katika mkutano wa Jumapili waoneshe mfano mzuri kama  wa Equatorial Guinea na kuwataka kujifunza kutokana na kupoteza mechi kwa timu kubwa kama Senegal iliyofungwa Zambia akawataka kuwa makini na kutowadharau wapinzani wao ambao wanashiriki mashindano hayo ambayo ni ya 28 kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment