13 October 2011

Yanga yampigia 'magoti' Manji

Na Suleiman Mbuguni

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umwendikia barua aliyekuwa mfadhili wao, Yusuf Manji ili arudi tena kuokoa jahazi.Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa
Yanga, Lloyd Nchunga alisema Manji kujiweka pembeni ameacha pengo kwani tangu alipoondoka hakuna mfadhili mwingine yeyote aliyejitokeza.

"Napenda kuwaeleza kwamba tumekuwa na majadiliano ya muda mrefu na mfadhili wetu wa zamani, ndugu Yusuf Manji ambaye alijitoa katika kuifadhili klabu na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida mtiifu.

"Hili limetokana na ukweli kwamba pengo lake limekuwa ni dhahiri katika kuiendeleza Yanga, na kipindi chote alichoondoka hakuna mfadhili wa aina yake aliyewahi kujitokeza japo wakorofi wachache walimbeza," alisema Nchunga.

Alisema ingawa wana mikakati endelevu ya kujitegemea kama kuuza vifaa vyenye logo ya Yanga, ambapo wameingia mkataba na Kampuni ya Nsejjere Sports Wear, lakini bado wanamhitaji Manji kwa kuwa ndiye amekuwa chachu ya maelewano na maendeleo ndani ya klabu hiyo.

Nchunga alisema anawaomba wana-Yanga kuonesha upendo kwa Manji ili aweze kurudi na kuifadhili tena klabu hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema katika ufadhili wake Manji, alichangia mambo mengi makubwa ndani ya Yanga, ikiwemo kuleta muafaka uliodumu kwa kipindi kirefu.

Alisema ana imani Manji atakubali ombi lao kwa kuwa katika majadiliano naye, alionekana kukubali lakini ametaka muda wa kulitafakari na kupata ushauri kutoka kwa familia yake na watu wake wa karibu.

Alisema hata hivyo, Manji ametaka kukutana kwanza na Kamati ya Utendaji ya Yanga, ili kuwekana mambo sawa.

"Hivi sasa Manji hayupo nchini, yupo Marekani lakini atakapokuja nitawaomba wana-Yanga kwenda kumpokea na kumkaribisha kwa upendo kwa kuwa anarudi na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa," alisema.

Alisema kwa wale wanaotaka kwenda kumpokea uwanja wa ndege kesho, wanaweza kufanya hivyo.

4 comments:

  1. Hivi Mungu sisi tumemkosea nin mpaka anatulaani hivi? Kwa nini tunaweka maisha yetu yote mikononi mwa watu badala ya kutumia majaliwa aliyotupa Mungu kujiendeleza? Ninyi viongozi wa yanga acheni kuidhalilisha timu na watanzania wanoipenda yanga. Mumefikiri kidogo kuhusu uwezekano wa Manji, kama binadamu wengine kufa? Mtamlilia nani? Hivi kweli mumetumia uwezo wenu wote wa kufikiri na kushauriana namna ya kuindesha timu, mkafikia hapo pa kujiweka watwana wa Manji. Mbona kikwete ni shabiki mkubwa wa yanga, kuna mama Karume kule Zanzibar na watanzania wengi wanaoweza kuichangia yanga ikajiendesha kwa heshima badala ya kuishi kwa kumwabudu Manji. Hivi mnadhani huyo Manji huo uwezo aliupataje? Jaribuni kuthubutu, msitake njia rahisi zinazowafanya msiwe na uhakika hata wa siku ya kesho. Inaniuma sana kuona jinsi tunavyonogea na ukoloni. Let us try to make a do with the little we have to preserve our respect instead of surrendering so easily into the hands of the haves who will not guarantee our tomorrow. Kwa nini? Why?

    ReplyDelete
  2. Mengi aliwaambia timu iwe kampuni ili iwezekujiendesha kisasa kama timu nyingine za Afrika kaskazini na Afrika magharibi mkafukuza na marungu na Manji alishawaeleza kitu hichohicho lakini bado hamkubali hasa wale wanaojiita ni wazee na waazilishi wa Yanga ndio wenye matatizo siku zote.Badala ya wao kuwa msaada kwa timu wanakuwa ni mzigo kwa timu kwa kunyemelea mapato ya mlangoni na nihodari sana kwa majungu watu hawa.Timu haiwezi kuendeshwa hivyo hata siku moja,Timu inatakiwa iendeshwe kisasa kwani soka inatakiwa iendeshwe kibiashara ndio mambo yataenda vizuri na sio kuwa ombaomba kila siku.

    ReplyDelete
  3. hiyo ni aibu jamani,klabu kubwa mmekuwa tegemezi kiasi hicho?kuweni wabunifu.

    ReplyDelete
  4. huu ni ujinga,yanga,simba jamani lini mtaacha kuabudu watu,Dunia imebadilika sana nyie vipi mbona hamuweji kabisa kubadili uendeshaji wa hizo timu.inaudhi kweli tena sana tu,haya kampigieni magoti tena na tena

    ReplyDelete