Na Heri Shaaban
TAWI la Simba la 'Wekundu wa Msimbazi' lililopo kituo kikuu cha mabasi ya mikoani Ubungo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
wamechagua viongozi wapya watakaoongoza tawi hilo.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa tawi hilo, Dar es Salaam jana Justine Mwakitilima, alizitaja nafasi zilizogombaniwa kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Katibu Msaidizi, Mhazini Mkuu na Mhazini Msaidizi.
Aliwataja aliochaguliwa kulioongoza tawi kuwa ni Martin Kumalija aliyekwaa nafasi ya Mwenyekiti, Absheikh Mchomvu Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu yeye mwenyewe na Katibu Msaidizi ni Julius Kiwale.
Katibu huyo alisema nafasi ya Mhazini Mkuu ilinyakuliwa na Havintishi Ngwele ambaye atasaidiwa na Gerge Mbegalo.
Alisema uzinduzi rasmi wa tawi hilo unatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Mwakitilima alisema tawi hilo lilianzishwa Februari mwaka huu ambapo wamepanga kufikisha wanachama 200, watakaoweza kuisaidia timu yao ya Simba ambayo inakabiliwa ana michuano mbalimbali.
No comments:
Post a Comment