17 October 2011

Extra Bongo yateka mashabiki Mbeye

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MAMIA ya wakazi wa jiji la Mbeya, juzi wamejitokeza kwenye tamasha la Kili Jivunie uTanzania, ambalo lilipambwa na bendi ya
Extra Bongo ikiongozwa na Ally Choki.

Tamasha hilo, lililoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambalo linaenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Uhuru, zilitanguliwa na maandamano ya amani kutoka Mbeya Mjini, kupitia Soweto hadi viwanja vya CCM Ilomba, ambapo kulikuwa na burudani lukuki.

Mamia ya watu walianza kufurika katika viwanja hivyo kuanzia saa tano asubuhi, huku wengine wakiufuata msafara mkubwa wa maandamano uliozinduliwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anaclet Marindisa.

Akizungumza katika tamasha hilo Kamanda Marindisa, ambaye alikuwa mgeni rasmi aliishukuru Kampuni Bia Tanzania (TBL) kwa kubuni kampeni ya Jivunie uTanzania ambapo alisema itawasaidia Watanzania kutafakari walikotoka na wanakokwenda.

“Kumekuwa na changamoto nyingi katika miaka 50 ya Uhuru wa Tangayika iliyopita na sasa hivi lazima tujiulize tutafanya nini huku tunakokwenda,” alisema.

Naye Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema Watanzania wana mambo mengi ya kujivunia katika miaka 50 ya Uhuru ikiwemo amani, upendo na lugha ya kiswahili ambavyo vimewaunganisha Watanzania.

Alisema matamasha kama hili tayari yamefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Katika tamasha hilo, bendi ya Extra Bongo chini ya Choki na Ramadhan Masanja 'Banza Stone', ilikongo nyoyo za mashabiki wa dansi waliofika katika viwanja vilivyo.

Katika hatua nyingine, kampuni mbalimbali ambazo ni marafiki wa TBL, yalishiriki katika mchuano wa mpira wa miguu uliochezwa kwa mfumo wa Simba na Yanga, ambazo ni klabu zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro.

Timu zilizoshiriki ni TBL, Vodacom, Pepsi, Mbeya Cement, Zantel na Mkon’goto.

No comments:

Post a Comment