Na Zahoro Mlanzi
WABUNGE wanne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wameibukia katika Kamati mbalimbali mpya za Klabu ya Simba, zilizoundwa
kushughulikia masuala ya uwekezaji na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu hiyo.
Wabunge hao ni Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Amos Makalla Mbunge wa Mvomero, Richard Ndassa Mbunge wa Sumve na Muktadha Mangungu Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
Mbali na hilo, klabu hiyo pia imepanga kuvunja jengo lao la sasa lililopo makao makuu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam na kujenga ghorofa la ghorofa 12.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage alisema mwezi mmoja uliopita walivunja Kamati ndogondogo, ili wapate nafasi ya kufanya kazi vizuri zaidi lakini hivi sasa wameamua kuja na kamati nyingine ambazo ni maalumu.
"Katika kikao chetu cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Oktoba 15, mwaka huu tulikubaliana kuwa na Kamati Maalumu za Ufundi, Mashindano, Fedha, Usajili na Nidhamu zikiwa katika sura na mitizano tofauti," alisema Rage.
Alisema kwa upande wa Kamati ya Fedha itakayoongozwa na Mwenyekiti, Geofrey Nyange 'Kaburu' akisaidiwa na Adam Mgoyi na wajumbe ni Mbunge Zitto, Juma Pinto, Said Pamba, Abdul Mtengeta na Mbunge Mangungu na Kamati ya Nidhamu itaongozwa na Peter Swai, Jamal Rwambow, Charles Keyela, Chaurembo na Evody Mmanda.
Alisema Kamati ya Mashindano itakuwa chini ya Joseph Itangile akisaidiwa na Azim Dewji, Jerry Ambi, Swedi Nkwabi, Mbunge Ndassa, Hassan Othman 'Hassanoo', Mohamed Nassor na Mbunge Makalla.
Kwa upande wa Kamati ya Ufundi, Rage alisema itaongozwa na Ibrahim Masoud 'Maestro', Danny Manembe, Khalid Abeid, Musley Ruwehi, Said Tuli, Mulamu Nga'mbi, Rodney Chiduo na Patrick Rweyemamu.
Kamati ya Usajili itakuwa na Zakaria Hanspope (Mwenyekiti), Kassim Dewji, Francis Waya, Salim Abdallah, Gerald Lukumay, Collins Frisch na Crensencius Magori.
Alisema tayari viongozi hao wameshapatiwa taarifa na kwamba jana jioni alitarajia kukutana nao ili kubadilishana mawazo na kupeana majukumu.
Katika hatua nyingie, Rage alisema wameshaanza kufanya mazungumzo na benki mbili juu ya kuziomba msaada, ili kusaidia kujenga ghorofa refu zaidi.
Alisema jengo lao la hivi sasa halina hadhi ya timu hiyo na kwamba, wana mpango wa kutengeneza jengo la ghorofa 12 kwenda juu.
Huo ni mwanzo mzuri kama hayatakuwa maneno matupu Bwana Rage maana tunataka klabu zetu zisiwe tegemezi kwa kila kitu hongera sana na wale wote waliochaguliwa fanyeni kazi.
ReplyDelete