Na Zahoro Mlanzi
UONGOZI wa Klabu ya Simba, umefungua milango kwa timu yoyote inayomhitaji beki wao 'mtukutu', Kelvin Yondani kumsajili
wawasilishe maombi rasmi kwao.
Mbali na hilo, uongozi huo umemtaka beki huyo aweke wazi hatima yake ya kuichezea timu hiyo kwa barua kuliko kukaa kimya na kuendelea kuonesha utovu wa nidhamu kwa timu hiyo.
Beki huyo tangu agomee mazoezi, amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kwenda kuimarisha safu ya ulinzi inayoonekana kupwaya katika mechi mbalimbali za ligi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa timu hiyo Ismail Rage, alisema wanashangazwa na ukimya wa beki huyo licha ya kumwandikia barua mbili za kujieleza, kwanini hajatokea mazoezini kwa wiki nne.
"Unajua mkataba wa mchezaji na klabu ni sawa na ndoa ya mke na mume na ndiyo maana hata wazee wetu walituasa kwamba tuwe wavumilivu katika ndoa na ndiyo maana na sisi tunaendelea kumvumilia kwa kumwandikia barua, lakini ikifika ya tatu akiendelea kukaa kimya tutajua la kufanya," alisema Rage.
Alisema wanasikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama mchezaji huyo, anataka kuhama lakini wanamwomba afuate taratibu husika na pia timu inayomhitaji ijitokeze wafanye nayo mazungumzo.
Aliongeza si kwa beki huyo, ila ni kwa mchezaji yeyote ambaye anaona amechoka kuitumikia timu hiyo, awasiliane na uongozi kuliko kwenda kinyume na taratibu zao.
Wiki iliyopita klabu hiyo ilisitisha kumlipa mshahara wa mwezi uliopita, ikiwa ni hatua za awali ambazo wameanza kuzichukua kutokana na mwezi huo kutoufanyia kazi.
simba inapenda sana kuwadhulumu wachezaji, si mnakumbuka ya Banka? au Chuji? yanga wamwacha kwa ukutuku wao wakampa tamaa then baadae wakamtosa.
ReplyDeleteZahoro be specific don't talk no sense.
ReplyDelete