10 October 2011

Wabunge CHADEMA kortini leo

Na Moses Mabula, Tabora

KESI inayowakabili wabunge wawili wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) na mjumbe mmoja wa Baraza la Vijana la chama hicho leo itatajwa katika Mahakama ya Mkoa wa Tabora wakikabiliwa na mashtaka manne.
Wabunge hao ni Bw. Sylvester Kasulumbai wa Jimbo la Maswa- Mashariki na Bi. Suzan Kiwanga, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro na Bw. Anwar Kashaga ambaye ni mjumbe wa baraza la vijana CHADEMA wilaya ya Igunga.

Septemba 19 mwaka huu watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao na kuyakana mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mkoa wa Tabora, Bw. Thomas Simba.Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka Bw. Juma Masanja akisaidiwa na Mugisha Mbonea alidai kuwa mnamo Septemba 15, mwaka huu majira ya mchana huko katika Kijiji cha Isakamaliwa wilaya Igunga, mshtakiwa wa kwanza, Bw. Kasulumbai alitoa lugha ya matusi kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatuma Kimario.

Aliendelea kwamba mshtakiwa huyo alisema: "Malaya mkubwa, huyu ndiye niliyetaka kuzaa naye mpumbavu mkubwa, DC gani huyo hana akili?.

Ilidaiwa kuwa huko katika Kijiji cha Isakamaliwa Wilaya ya Igunga washtakiwa kwa pamoja walimshambulia Bi. Kimario na kumsababishia maumivi ya kichwa.Katika kosa la tatu washtakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kumshikilia Bi. Kimario bila uhalali na kinyume cha Sheria kifungu namba (253) kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kosa la nne wanalodaiwa kutenda watuhumiwa hao kumwibia Bi. Kimario dimu ya mkononi aina ya Samsung yenye thamani ya sh. 400,000.

Upande wa utetezi unaongozwa na mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lisu akisaidiwa na wakili wa kujitegemea, Bw. Musa Kwikima. Wote walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru hadi leo.
Watuhumiwa hao walikamatwa na polisi mjini Igunga wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Septemba 16 na kuhojiwa, na siku iliyofuata walikamatwa tena na kuhamishiwa mjini Tabora ambako walifikishwa mahakamani.

2 comments:

  1. Nimesoma vizuri hata ya mashitaka! Ila nimeshtuka kutoona kosa la kumvua HIJAB Bi Fatma Kimario, ambalo ni kuudhalilisha uislamu.

    BAKWATA sijui wanasemaje kuhusu makosa ya walalamikiwa? Je Kutotatajwa kosa la kuvuliwa HIJAB na haukuwezi pia kutafisiliwa kuwa ni mwedelezio wa kudhalilisha uislamu. Kwa matazamo wa waendesha mashitaki it is a non-isuue ndiyo maana was not mentioned at all?

    Sheihk Mkuu Shaaban Bin Simba tunaomba mwongozo wako kuhusi hii hata ya mashitaki.

    ReplyDelete
  2. Ww mwananchi usiena na jina,Ninakukumbusha tu Bi.Fatuma sio Mwislam alisilimu baada ya kuoelewa na Mkristo.Ninakupa taarifa fupi ya Bi.Fatuma Kimario.
    Na istoshe inchi yetu haitawaliwi na Kidini.
    Huyo aliekudanganya kuwa Sheikh Mkuu anaubavu kisheria amekudanganya,Hilo ndio tatizo la Waislam.
    Kwa shauri njoo kwa Yesu iliupate uzima wa Milele.

    ReplyDelete