Na Amina Athumani
KLABU Gymkhana ya Dar es Salaam, imewaomba Watanzania kujitokeza katika viwanja hivyo, kujifunza mchezo wa skwashi ambao kwa
kiasi kikubwa bado haujapata wapenzi.
Rai hiyo ilitolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mtendaji Mkuu wa Klabu Gymkhana, Dicholaus Siwingwa ambaye pia amewataka waandishi wa habari kuupigia debe kwa Watanzania, ili uweze kutambulika.
"Gymkhana tuna michezo mingi, lakini tunashangaa kuona Watanzania wengi hawaji kujifunza mchezo huu, jambo ambalo unaonekana kama vile haupo," alisema Siwingwa.
Alisema wao kama Gymkhana, wamejipanga kuhakikisha mchezo huo unapata sehemu nyingi za kuchezewa kama ilivyo michezo mingine.
"Mchezo huu huwa auhitaji sehemu kubwa ya kiwanja, ila ni kichumba kidogo tu ambacho huwekwa vifaa na watu wakaweza kucheza," alisema.
Alisema pia wadau wanatakiwa kujitokeza kutoa sapoti zao katika mchezo huo, ikiwemo kununua vifaa vingi vya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment