Na Patrick Mabula, Kahama
OFISI ya serikali Kata ya Malunga Wilayani Kahama imenusurika kuungua baada ya kuchomwa moto usiku wa manane na watu wasiojulika kutokana na tofauti za kisiasa za viongozi
wa CCM ndani ya kata hiyo.
Ofisi hiyo ilimwagiwa mafuta taa na kuchomwa moto usiku wa manane siku ya
Jumapili kabala ya watu wanaoishi karibu na eneo hilo kuona moto ukianza kuwaka sehemu ya mlango wa mtendaji wa kata hiyo na kupiga kelele.
Mtendai wa Kata ya Malunga Bi.Sesilia Clement, alisema jana kuwa wachomaji hao kwanza walikusanya karatasi za plastiki na kuziweka katika mlango wa ofisi yake kisha wakamwaga mafuta ya taa na kuzichoma moto lakini wananchi waliwahi na kuuzima.
Wakisumulia tukio hilo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema hatua hiyo ilisabishwa na tofauti za kisiasa.
Bw.Williamu Masalu, alisema tangu uchaguzi umalizike mwaka jana katika kata hiyo kumekuwepo tofauti za kisiasa zinazosababisha matukio ya aina hiyo baada ya Chama Cha Wananchi (CUF) kuibuka na ushindi katika kata hiyo dhidi ya CCM.
No comments:
Post a Comment