28 December 2010

Tofauti ya kura 1% yamliza Seif

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho kukaa chini na kutafakari kwa namna gani waliikosa asilimia moja ya kura, ambayo iliwapatia
ushindi CCM katika uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu.

Tamko hilo alilitoa juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Nungwi Wilaya ya Kaskazini  Unguja, ambao uliandaliwa maalumu kwa ajili ya kupongezana.

Alisema kuwa katika uchaguzi huo CCM ilishinda kwa asilimia 50.1 na wao wakapata asilimia 49.1, jambo ambalo alisema wanapaswa kuliangalia kwa kina na kulipatia ufumbuzi wake.

Katika uchaguzi huo tulitarajia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi, lakini tulizidiwa na wenzetu na hatimaye tukashindwa kwa asilimia hiyo moja, suala hili tunapaswa tukae na kujiuliza ni kwanini tuliikosa asilimia hii,” alieleza.

Ushindi ni ushindi hata uwe wa asilimia moja kwa vile nchi yetu inaongozwa na katiba, hivyo ni wajibu wetu kujiuliza hii asilimia moja tumeikosa vipi, na tujipange si kwa kuitafuta asilimia moja pekee bali tujiandae kwa ushindi wa asilimia 71, aliongeza.

Aliwataka viongozi na wanachama hao wasije wakaridhika na hatua iliyopo na badala yake wajipange ili kukiimarisha chama chao, kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Maalim Seif alisema akiwa katibu wa chama hicho amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara katika majimbo na matawi ili kuwakumbusha namna ya kupanga mikakati ambayo itawasaidia katika kukipatia ushindi chama chao.

Tusije tukaona kwamba muda bado ni mrefu kwa sababu nguo ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi lakini nayo inaweza kuwa na mawingu kwa hivyo fueni Jumatatu,” alisistiza maalimu.

Alieleza kuwa siku zote chama kinakuwa na malengo yake maalumu ambayo kimejiwekea, yanapaswa kutekelezwa ili kuyafikia.

Alisema kuwa katika mfumo wa serikali chama kina umuhimu wake kwa sababu ndicho kinachochagua viongozi na kuunda serikali, hivyo katika mfumo huo huwezi kukidharau chama hicho.Wakati wote tusisahau kwamba chama kina sera zake, malengo yake na makusudio yake ambayo kutekelezwa kwake ni lazima kiwemo kwenye serikali, alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa kama chama kinataka kutekeleza hilo ni lazima kufanywe kazi na kupata kura nyingi ili kuongoza serikali yenyewe.

Aliwataka viongozi hao pamoja na wanachama wajipange kwa uchaguzi ujao kwa kuhakikisha kuwa chama chao kinashinda hasa kwa vile bado wananchi wa Zanzibar wanahitaji kuongozwa na CUF.

6 comments:

  1. Ndugu zangu mlikubali tu kwakuwa ulijua utakuwa makamu wa kwanza wa raisi otherwise sidhani kama ungeweza kukubali matokeo kirahisi hivyo kwa kushindwa kwa asilimia moja tu!!!!!!
    Hii inadhihirisha jinsi gani tanzania hatuna viongozi bali tuna waroho wa madaraka!!!!!!
    KWA JINSI HII JE TUTAFIKA KWELI!!!

    ReplyDelete
  2. WALA USIKONDE, ULIYATAKA MWENYEWE NA MUAFAKA WAKO ILI WEWE UPATA UMAKAMU. Wewe ndio utafakari, uwape jibu wenzako badala ya kuwazunguka na kuwatupia mzigo wa kutafakari madudu yako!

    ReplyDelete
  3. acheni coment za chuki watu wakiuuwana ndio raha yenu uroho wa madaraka hautusaidii kama hujui kifo chungulia kaburi SEIF Kafanya na MUNGU ATAMBARIKI safari hii hatujaumizana nyie mnaopenda watu wakiumizana hameni

    ReplyDelete
  4. Maalim Seif anatumia Balagha kufikisha ujumbe, kwani pamoja na kuibiwa kura kutoka CCM, pia kulikuwa na uzembe wa hapa na pale, kuanzia wapiga kura wa CUF na pia Mawakala. Kuna wanachama wa CUF hawakujiandikisha, na kuna wengine walijiandikisha lakini hawakwenda kupiga kura bila sababu za msingi. Huo ni ujumbe na mwenye akili ndio ataghamua madhumuni ya Maalim Seif.

    ReplyDelete
  5. Maalim akawaulize Mkapa na Mwinyi hiyo kura moja waliifisa wapi?. Na kwa taarifa wala si moja tu.

    Maalim atakatupumbaza sasa, mara moja hii keshasahau chaguzi za nyuma?!. Haa ntoka lini CUF ikashidwa?, ama Maalim nawe!.

    ReplyDelete
  6. AMA KWELI MAALIM KANSAHAUUUUU!!!!!! KASHASAHAU MARA HII MOJA JAMANI!!!!! AAAAH!!! SIASA JAMAA SI KAZI!!!.ivi maalim kunsahau kuwa Cuf hijapatapo kushindwa toka 1995? nawe pia ukitwambia hivo au nvipi tena?ee!! maalim kumbuka tulivyopambana mpaka tulipo sasa. mie nayamaza mana nkikumbuka hutamani lia.

    ReplyDelete