28 December 2010

Mahabusu wagoma, wavua nguo

Na Muhidin Amri, Songea

MAHABUSU wanaokabiliwa na kesi za mauaji wamegoma kupanda gari la polisi kurudi gerezani na baadhi yao kuvua nguo kwa madai ya kucheleweshewa upelelezi wa kesi zao zinazazowakabili.Tukio hilo lilitokea jana pale
mahabusu hao wapatao 20 walipotolewa na polisi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma, kurudishwa magereza kusubiri tarehe ya kusikilizwa kwa kesi zao.

Mahabusu hao walichukua hatua hiyo kwa madai ya kucheleweshwa kwa kesi zao ambazo ni za muda mrefu huku  wengine wakibadilishiwa kesi za awali na kusomewa mpya, tofauti na zile walizokamatwa nazo.

Akizungumza kwa niaba ya maabusu wenzake, Bw. Rashid Gayo alisema kuwa wamefikia uwamuzi huo baada ya kuchoshwa na tabia ya kucheleweshwa kwa kesi hizo ambazo ni za muda mrefu, huku wakimtuhumu kigogo wa polisi anayehusika kwa upeplelezi kwa kuwaomba rushwa.

Alisema kuwa lengo mgomo huo ni kutaka kufikisha ujumbe kwa vyombo vinavyohusika ili vichukue hatua zinazostahili.Alidai kuwa kigogo wa upelelezi mkoani humo amekuwa na tabia ya kuwaomba fedha ili kuharakisha upelelezi wa kesi zao, huku akifahamu kwamba uwezekano wao kupata fedha hizo ni mdogo.

Kamanda wa Polisi mkoa ni Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa mahabusu kugoma ni haki yao ya msingi lakini, kitendo cha kuvua nguo hakiwezi kuwa ndiyo sababu ya kuharakisha upelelezi wa kesi zinazowakabili.

Akisema mahabusu hao wameshawahi kugoma kula na alikwenda gerezani kuongea nao na aliwahaidi kuchukua hatua kuharakisha upelelezi huo, na kuwataka mahabusu hao kuwa kusubiri upelelezi wa kesi zao.Alisema jeshi lake halina namna ya kuwasaidia mahabusu hao, kwani hata majalada ya kesi zao bado yako kwa Mkurugenzi wa Mashataka (DPP).

1 comment:

  1. Suala la jeshi la polisi kwa Tanzania kuomba rushwa ni ugonjwa uliokomaa na hautatibika leo au kesho bila ya kuwa na Rais asiyependa uswahili na urafiki.Jeshi zima la polisi Tanzania lingefutwa na kuanza na askari wapya jeshi hili linanuka rushwa.Askari wa tanzania ktk jeshi la polisi ni wezi na wanapenda sana pesa ya rushwa.Wengi wa askari hao ni majambazi na serikali haijui wengi wa askari wa vyeo vya chini wananetwork kubwa na majambazi na kupata kamishen baada ya ualifu kufanyika.Wengi ni wanywaji wa pombe na uzinzi ni maisha yao na kubambika kesi watu ili wapate pesa.Jeshi la polisi limegeuzwa kuwa mradi kwa askari badala ya kufanya kazi yao ambayo ni kulinda usalama na mali za raia lakini imekuwa kinyume ni kunyang'anya mali za Raia na kuvuruga amani.Rais fukuza mkuu wa polisi na mkuu wa upelelezi,mkuu wa trafiki,mkuu wa magereza wanakula pesa za bure za walipa kodi.Rais kikwete acha uswahili na urafiki na watu wako wa karibu ndio maana wanakuangusha kkt kazi zao.Inabidi uwe tough kidogo kama IDD AMINI nchi inapotea na wezi unakaa nao hapo hapo na kucheka nao na wanakuona sio SMART kabisa try to be aggressive so folks they fed up with the entire system of yours.

    ReplyDelete