Rehema Mohamed na Salim Mhando
WATU wanne wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka ya kujipatia sh. milioni 50 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Bw. Suleiman Hamisi kwa kumuuzia kiwanja cha wakfu kinyume na utaratibu.Watuhumiwa hao ni
Kassim Astesh (40), Abeid Hamza (52)Bw. Thabit Machambo (40) na Hassan Ruvuka (35).
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Bi. Naima Mwanga alidai mbele ya hakimu, Bw. Karimu Mushi ilidaiwa kuwa walitenda kosa hilo Kinondoni Julai mwaka huu .
Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja waliuza kiwanja namba 83 jengo 'M' kilichopo Mtaa wa Kongo, Kariakoo mali ya Jamyat Islamia 'A' Tanganyika Muslim School wakijua kuwa ni mali ya waislam.
Katika kosa lingine ilidaiwa kuwa Septemba 22 mwaka huu watuhumiwa hao pia walighushi risiti namba 36510 ya malipo ya ardhi kutoka Manispaa ya Ilala kuwa wanakilipia kihalali kiwanja hicho, kwa lengo la kuthibitisha kuwa ni mali yao.Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walibadili dini kutoka ukristo kuja uislamu ili kukamilisha adhma ya kuuza jengo hilo.
Watuhumiwa wote wamekana mashtaka huku Bw. Thabiti Machambo akirudishwa rumande kutokana na kukosa wadhamini, wengine wapo nje kwa dhamana. Kesi imehairishwa hadi Desemba 16, mwaka huu.
Wakati huo huo wakazi watatu wa Temeke wamefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za mauaji ya watu wa wili, Bw. Fadhili Adam na Bw. Mussa Said maarufu kama ustadhi.
Watuhumiwa hao ni Bw. Mwinyi Mzurika (29), Bw. Mohamed Nasori (28) na Bw. Mbwana Kisena (29).Mwendesha Mashtaka, Bi. Naima Mwanga alidai mbele ya hakimu Bw. Karim Mushi kuwa wafanya mauaji hayo Mei 18, mwaka huu saa 1 jioni eneo la Vingunguti Faru.
Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji. Kesi emeahirishwa hadi Desemba 16, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment