LONDON, England
MICHUANO ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, inatarajia kuendelea leo katika viwanja mbalimbali barani humo, huku baadhi ya vigogo vikiwa vimeshafuzu hatua ya mtoano.Katika mfululizo wa michuano hiyo, Barcelona watakuwa wakiikaribisha
Rubin Kazan, katika mechi za kundi D huku Benfica wao wakiumana na timu ya Schalke 04 katika mechi za kundi B.
Wakati miamba hiyo ikioneshana kazi, timu ya Bursaspor itakuwa wakioneshana kazi na timu ya Rangers, katika mechi ya kundi C na
FC Copenhagen, watakuwa wakitoana jasho na Panathinaikos katika mechi za kundi D.
Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya FC Twente itakayokuwa mwenyeji wa Tottenham, wakati Lyon wao watatoana jasho na Hapoel Tel-Aviv huku Manchester United watakuwa nyumbani wakiumana na Valencia na timu ya Werder Bremen watakuwa wakikabiliana na Inter Milan katika mechi za kundi A.
Timu za Chelsea na Marseille zenyewe zimeshafuzu kutoka kundi F, wakati Real Madrid na AC Milan nazo zikiwa zimefuzu kutoka kundi G.
No comments:
Post a Comment