Na Amina Athumani
MASHINDANO ya kuibua vipaji vya muziki wa dansi ya 'Dance Music Competition', yanatarajia kuanza Desemba 20 na 21 mwaka huu katika Ukumbi wa Africenter, Dar es Salaam.Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo ambaye pia ni nguli wa
muziki huo, Ali Choki alisema mchuano huo utakuwa wa kihistoria na yataibua vipaji vingi vya vijana.
"Tunataka kuona akina Ali Choki, wengi wanapatikana kupitia mashindano haya na sisi tukiwa kama wadau wa muziki na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuyaunga mkono mashindano haya ili yaweze kufanikiwa zaidi.
"Hakuna mpenzi yeyote wa muziki wa dansi atakayekosa jibu kuwa ni kwa namna gani wanamuziki kama Marijani Shaban, John Kijiko, Mbaraka Mwishehe, Mzee Makassy, Mzee Ngurumo na wengineo walivyoutukuza na kuukuza muziki huu, hivyo kwa kuwa muda unasogea wanahitaji wabadala wa muziki wao," aliongeza Choki.
Alisema vijana watakaoingia katika fainali hizo, watapelekwa kambini ambako watafundwa na walimu mbalimbali wa muziki, ikiwa ni pamoja na kupewa semina mbalimbali za muziki huo.
No comments:
Post a Comment