LONDON, Uingereza
CARLO Ancelotti amekiri anahisi kuwa katika wakati mgumu, kulinda kibarua chake.Mabingwa watetezi Chelsea, wamepungua makali yao ambapo katika mechi sita wameshinda moja tu.Kocha huyo wa Blues, amekiri kuwa hatima yake ya baadaye kwenye klabu hiyo, imeingia
kiwingu kutokana na Chelsea kupata mtokeo mabaya zaidi katika kipindi chake cha miaka 10 ya ukocha.
Ancelotti alisema: "Si maamuzi yangu, ni maamuzi ya klabu."Kwa kawaida unapokuwa na wakati mgumu ni wakati ambao hutafutwa ni nani wa kumlaumu. Lakini hatutafuti mwenye makosa."Ancelotti amekuwa akiwalaumu wachezaji wake kwa kucheza chini ya kiwango, katika mechi za karibuni ambapo wamepata pointi tano kati ya 18.
Rekodi yake katika mechi sita za Ligi Kuu ni mbaya zaidi kuliko makocha sita waliofanya kazi chini ya Roman Abramovich kwenye klabu hiyo.
Avram Grant alioneshwa mlango wa kutokea akiwa ameshinda mechi kwa asilimia 67, katika mechi zake sita za mwisho karika Ligi Kuu, ikiwemo kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutolewa kwa penalti dhidi ya Machaster United mjini Moscow.
Ilishinda mechi dhidi ya Fulham na kufungwa ugenini na Liverpool na Birmingham, na ikaja kufungwa mabao 3-0 dhidi na Sunderland na kutoka sare dhidi ya Newcastle na Everton.Ancelotti alisisitiza: "Tatizo liko uwanjani na si kwenye benchi."Aliongeza: "Ninajaribu kusisitiza hali ya kujiamini miongoni mwa wachezaji. Ninaongeza hali ya kuwaamini lakini si wakati mzuri na si kwao wala kwangu.
Alisema timu hiyo inatakiwa kucheza soka yake, kucheza kwa ushindani katika Ligi Kuu.Lakini presha imekuwa kubwa kwake kiasi kwamba hapati usingizi mzuri.Baada ya timu yake kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton, alisema: "Hali si nzuri, sina raha na pia silali vizuri."Chelsea bado inakabiliwa na mechi ngumu ugenini dhidi ya Tottenham, nyumbani na Manchester United na ugenini tena dhidi ya Arsenal.
Lakini mshambuliaji Didier Drogba, ambaye alifunga goli la penalti dhidi ya Toffees, alisisitiza kuwa atajitahidi kuiokoa timu.
No comments:
Post a Comment