Na Mohamed Akida
TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya AFC Arusha jana iliinza vyema michuano ya Uhai Cup, baada ya kuifunga timu ya vijana ya Polisi Tanzania mabao 2-0, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume.Michuano
hiyo ambayo inashirikisha timu za vijana za klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo inafanyika kwa mara ya tatu msimu huu.
Katika mchezo huo timu zote ziliuanza mchezo huo kwa kasi, huku zikishambuliana mara kwa mara na kushuhudia washambuliaji wa pande zote mbili wakipoteza nafasi nyingi za wazi, hivyo kufanya timu hizo kwenda mapunziko bila kufungana.
Kipindi cha pili, Polisi Tanzania walikianza kwa kulishambulia lango la AFC, lakini mshambuliaji wake Keneth Abed alikosa bao la wazi dakika ya 59.
Baada ya kusakosa hizo, AFC ilitulia na kupanga mashambulizi kwa makini, ambapo dakika ya 71 ilijipatia bao la kuongoza lililofungwa na Jamali Fadhili kwa shuti kali akiunganisha krosi ya Zakayo Joseph.
Bao hilo liliiongezea kasi ya mchezo, AFC na kuanza kulishambulia mfululizo lango la Polisi na dakika ya 80, Jeseph Msafiri aliifungia bao la pili timu yake baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Polisi.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuendelea tena jana jioni kwa timu ya Ruvu Shooting kupambana na Mabingwa watetezi Azam FC kwenye uwanja huo wa Karume.
No comments:
Post a Comment