Na Addolph Bruno
TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar, imetamba kutwaa tena ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 'Mapinduzi Cup' ambalo michuano yake itaanza kutimua vumbi Januari 2, mwakani mjini Zanzibar.Akizungumza kwa simu jana, Kocha Msaidizi wa
timu hiyo, Mecky Mexime alisema kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha na wana uzoefu wa kutosha katika mashindano hayo.
Alisema kutokana na uzoefu na nia waliyonayo, watakwenda kushindana kuhakikisha wanatwaa tena ubingwa wa michuano hiyo msimu huu.
"Kwa ujumla maandalizi yetu yanaendelea vizuri, kikubwa ni kwamba tunaenda kushindana, hatuendi kushiriki kwa sababu tuna nia ya kuutetea ubingwa wetu," alisema Mexime.
Kocha huyo alisema timu yake inatarajia kuondoka Januari Mosi, mwakani kwenda visiwani humo kwa ajili ya mashindano hayo.
Michuano hiyo inatarajia kushirikisha timu za Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar kwa upande wa Tanzania Bara, wakati Zanzibara kuna timu za Zanzibar Ocean View, KMKM na Polisi.
No comments:
Post a Comment