Na Eliasa Ally, Iringa
ZAIDI ya sh. milioni 60 zitatumika kujenga Tawi Benki ya NMB katika eneo la Gangilonga katika Manispaa ya Iringa.Akizungumza ofisini Majira Meneja wa Benki ya NMB Tawi la
Mkwawa Mkoa wa Iringa Bw. Atupele Mwakibete alisema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuihamisha benki ya sasa ambayo itabomolewa na kujenga jengo la kisasa zaidi katika eneo hilo.
Bw Mwakibete alisema kuwa ujenzi wa benki hiyo utachukua miezi sita hadi kukamilika Alisema kuwa mkoa wa Iringa sasa umekuwa na kuzaa mkoa mwingine wa Njombe hivyo na NMB inatakiwa kupanua wigo wa huduma zake.
Bw. Mwakibete alisema kuwa benki hiyo inatarajia kujenga klabu kubwa ya wateja wa wake ambayo itakuwa na kazi yake kutoa ushauri kwa benki hiyo ili itoe
huduma bora zaidi kwa wateja wake kufuta kero zinazowakabili.
"Tumejipanga na nitahakikisha ujenzi wa benki hiyo mpya unakamilika na uanzishwaji wa klabu hiyo kubwa ya NMB ya Mkoa wa Iringa inakamilika na nitahakikisha kunakuwepo na mafanikio makubwa zaidi na wateja wetu wananufaika zaidi kwa misaada, mikopo pamoja na huduma zingine za kibenki wanazohitaji,"alisema
No comments:
Post a Comment