KHARTOUM, Sudan.
MABINGWA watetezi wa michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) itakutana uso kwa uso na timu za Ivory Coast, Cameroon na
Mali katika fainali hizo zitakazofanyika Februari nchini Sudan.
Kwa mujibu wa droo, iliyofanyika Jumamosi mjini Khartoum wenyeji wa michuano hiyo wamepangwa kundi A wakiwa na timu za Gabon, Uganda na Algeria.
Ghana, Afrika Kusini, Zimbabwe na Niger zimepangwa kundi moja huku kundi la mwisho likiwa na timu za Senegal, Rwanda, Angola na Tunisia.
Mashindano hayo yanayofahamika kama CHAN, yataanza kutimua vumbi kuanzia Februari 4 hadi 25, mwakani.
Mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka jana nchini Ivory Coast, yalizihusisha timu nane lakini safari hii mashindano yameongezewa timu na kufikia timu 16.
No comments:
Post a Comment