LONDON, England.
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham na mkewe, Victoria ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuwapongeza wachumba wa familia ya kifalme kwa kuvalishana pete ya
uchumba wiki iliyopita.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya nyumba hiyo ya kifalme vilieza kuwa Beckham, alimtumia ujumbe Prince William wa kumpongeza muda mfupi baada ya kusikia taarifa hizo za kuvalishana pete ya uchumba.
“David alimtumia ujumbe wa pongezi Wills muda mfupi baada ya kusikia taarifa hizo na Wills akamweleza kuwa mwaliko upo njiani, David na Victoria wote walifurahi sana na hawakuweza kusubiri,” vyanzo hivyo vya habari kutoka ndani ya nyumba hiyo ya kifalme vilieza.
Kwa mujibu wa taarifa za vyanzo hivyo, David (35) na mwanamitindo Victoria (36) wataungana na orodha ya watu nyota watakaohudhuria sherehe hiyo, itakayofanyika katika eneo la Westminster Abbey April 29, mwakani wakiwemo, Sir Elton John na Sir Paul McCartney.
Mbali na wageni hao, Rais Obama na mkewe Michelle pia wamo kwenye orodha ya wageni hao, ambayo inatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa Februari, baada ya wachumba hao kukamilisha kila kitu.
No comments:
Post a Comment