LONDON, Uingereza.
MAROUANE Chamakh ameingia katika kundi la majeruhi, ambapo atalazimika kukosa kucheza mechi kadhaa.Mshambuliaji huyo wa Arsenal, alifunga bao lake la 10 katika msimu wake wa
kwanza, akiwa England kwenye mechi dhidi ya Aston Villa Jumamosi.
Aliumia bega na kupata maumivu ya shingo na sasa hatacheza katika mechi ya michuno ya Kombe la Ligi, wakati Arsenal itakapocheza na Wigan.
Mchezaji huyo kutoka Morocco, ambaye alihamia Arsenal akitoke Bordeaux, alisema: "Sikuwahi kuwa katika hali hii Bordeaux.
"Mambo yamekuwa tofauti hapa. Dhidi ya West Ham nilipata maumivu makali katika shingo yangu.
"Ilikuwa ni ngumu kugeuza kichwa changu."
Alisema amekuwa na wakati mgumu katika mechi hiyo kuchezewa vibaya na mwamuzi kutopuliza filimbi.
"Wakati watu walipokuwa wakinisukuma Ufaransa, nilianguka na kupewa adhabu. Wakati ninapochezewa faulo hapa ninatakiwa kusimama na kuendelea kucheza.
"Baada ya mechi ya Ligi Kuu, natoka uwanjani huku mwili wangu ukiuma, misuli ikiuma. Siku tatu baadaye unaendelea kucheza.
No comments:
Post a Comment