Na Jamillah Daffo, Manyara.
JESHI la Polisi linamshikilia Bi. Jenipher Kitundo mkazi wa Kitongoji cha Lamai–Kateshi wilayani Hanang kwa tuhuma ya kujifungua na kutupa kichanga kwenye banda la mbwa.Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Aurelia Msindai, tukio hilo lilitokea Novemba 26 mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku.
Kamanda Msindai alisema kuwa mwanamke huyo ambaye ni
mtumishi wa kazi za ndani katika nyumba ya Bi. Rutha Isindo (33), alijifungulia bafuni kisha kumtupa kumtupa mtoto katika banda la mbwa nyumbani hapo.
Alisema kuwa kichanga hicho kililiwa na mbwa na kusababisha kifo chake bila kufahamika jinsia yake kutokana na kuliwa maeneo mbalimbali zikiwamo sehemu za siri na kubakishwa kiwiliwili na kichwa.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Wakati huo huo mchimbaji wa madini ya Tanzanite, huko Songambele Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Bw. Selemani Ramadhani (29) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mfanyakazi wake wa ndani.
Kamanda Msindai alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 27, mwaka huu saa 1:15 katika mji mdogo wa Mirerani, Simanjiro.
Siku tukio mfanyakazi wa mchimbaji huyo aliyefahamika kwa jina la Sadiki au Kibweteke alimchoma kisu tajiri wake huyo sehemu ya tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje, kisha akamjeruhi mke wa marehemu kwa kumchoma kisu sehemu ya nyonga.
Majeruhi wote wawili walikimbizwa katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha, lakini Ramadhani alifariki juzi usiku wakiti akiendelea na matibabu.
Chanzo cha mauaji hayo, kwqa mujibu wa polisi, ni wivu wa
kimapenzi uliotokana na mfanyakazi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi wa mke wa Ramadhani, na alipogundua uhusiano huo, alileta zogo lililosababisha mtuhumiwa kuchukua uamuazi wa kuua.
Pia alisema kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na jeshi la polisi linaendelea kumtafuata ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment