26 August 2013

UTANDAZAJI BOMBA LA GESI KUANZA LEONa Godfrey Ismaley,Aliyekuwa Lindi
SERIKALI imeweka wazi kuwa kuanzia leo shughuli ya utandazaji wa bomba la gesi kutoka Mnazibay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam unaanza na inatarajia kabla ya Septemba mwaka huu litakuwa limekamilika
.Utandazaji wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 534 unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.2, zikiwa ni jitihada za Serikali za kutaka kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ambapo ziada itauzwa ili kukuza pato la taifa.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo aliyabainisha hayo mwishoni mwa wiki, baada ya majumuisho ya ziara maalumu ambayo aliifanya na waandishi wa habari Somanga Fungu mkoani Lindi ili kujionea namna bomba hizo zitakavyounganishwa leo.
Pia ziara hiyo ilimjumuisha Balozi wa China nchini, Lu Yonging ambapo kampuni za China Petroleum Technology & Development Corporation (CPTDC) na China National Petroleum Corporation (CNPC) zilishinda zabuni ya kusimamia utandazaji huo wa bomba chini ya usimamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).
Prof. Muhongo alisema kuwa, licha ya mradi huo wa kutandaza bomba la gesi kuongeza ajira kwa Watanzania, pia baada ya kukamilika unatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme mara mbili ya kiwango cha sasa ambacho ni zaidi ya Megawati 1,500 nchini kote.
" Tu n a omb a Wa t a n z a n i a waendelee kuvumilia na kuunga mkono mradi huu ambao tunaamini baada ya kukamilika kila mmoja ataona manufaa yake, kwa uchumi wa taifa na nishati ya umeme nchini," alisema Prof. Muhongo.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini, Lu Yonging alisema Watanzania wana kila sababu ya kujivunia rasilimali zao na kuunga mkono Serikali ili iweze kuzisimamia kwa manufaa ya taifa lote.
" P i a Ch i n a t ume j i t o l e a kuwachukua wasomi katika vyuo vikuu nchini Tanzania, ili waweze kwenda vyuo vikuu nchini China, kupatiwa ujuzi wa namna ya kusimamia rasilimali gesi asilia kupitia teknolojia ya kisasa. Tutazungumza na Wizara ya Nishati na Madini ili ituongoze namna ya kuwapata wasomi hao," alisema Balozi huyo.
Hata hivyo, gesi asilia ilianza kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974, kwenye Kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi huku mwaka 1982 ikigundulika Mnazi Bay na Ntorya mwaka 2012 mkoani Mtwara.
Aidha, mwaka 2007 iligundulika maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani na mwaka 2008 iligundulika tena eneo la Kiliwani mkoani Lindi ambapo kwa sasa gesi asilia iliyogundulika katika nchi kavu na baharini ni zaidi ya futi za ujazo trilioni 41.7.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, rasilimali gesi asilia inaweza
 kutumika katika maeneo mbalimbali kama kuzalisha umeme, mbolea, kemikali, nishati viwandani, majumbani na kwenye taasisi na kuendeshea magari

No comments:

Post a Comment