25 July 2013

MENO YA TEMBO YAMPANDISHA POLISI KIZIMBANI



Na Rehema Mohamed
ALIYEKUWA Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga, G 5226 PC Ramadhani Selemani (27), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu kazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 120.Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni mkazi wa Mbagala Zakhem, Hamis Mwanya (22).

Mbele ya Hakimu Nyigulila Mwaseba, ilidaiwa na Wakili wa Serikali Mwanaisha Komba, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 19, mwaka huu Tazara Wilaya ya Temeke.Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alikutwa na meno manne ya tembo pamoja na vipande 12 vya meno hayo mali ya serikali. Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu kosa hilo.Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba shauri hilo litatajwa tena Agosti 7, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment