21 January 2013

Kipindi hichi siyo cha msimu wa vyakula


Na Heri Shaaban

MFUMUKO wa bei katika bidhaa za vyakula Dar es Salaam unadaiwa kuwa unatokana na kipindi hichi kutokuwa cha msimu wa vyakula.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Meneja Mipango na Shuguli za Biashara Shirika la Masoko Kariakoo  (KMC) Mrero Mgeni wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea changamoto za Shirika hilo.

Mgeni alisema kuwa kupanda kwa bidhaa za vyakula katika masoko nchini kama mchele ,maharage,kunde,choroko na mahindi yanayozalisha unga sembe inatokana na wafanyabiashara wakubwa kununua vyakula hivyo kwa wingi na kuweka stoo.

"Kipindi cha mwezi Desemba na Januari hadi February sio kipindi cha mavuno hivyo wafanyabiashara wakubwa walikuwa wamenunua kwa wingi bidhaa hizo na kuzilimbikiza ndani, ambapo kipindi hichi wanazitoa na kupeleka sokoni,"alisema Mgeni.

Alisema kuwa pia kingine kinachosababisha kupanda kwa bidhaa katika masoko yetu ni kutokana na gharama za usafirishaji kuwa juu kutokana na bei ya mafuta aina msimamo ina cheza cheza.

Kuhusu changamoto za shirika hilo alisema kuwa miundombinu ya shirika hilo ya kizamani zaidi ya miaka 30 iliyopita, hivyo aliomba kuboresha ili iwe ya kisasa iweze kuvutia kama masoko mengine.

Pia alisema kuwa Shirika hilo linajiendesha wenyewe gharama za kulipia ushuru, pango na kodi ndio zinaendesha shirika.

Alisema kuwa kwa sasa wakulima wanalipia ushuru wa tenga moja na nyanya sh.600,gunia la viazi sh.800,pilipili sh. 1000,njegere,sh.800,dagaa wa Kigoma sh.1,500 na dagaa wa Mwanza sh.3,500 ili kupata fedha za kuendesha shirika.


No comments:

Post a Comment