20 December 2012

Mgombea Ubunge CHADEMA ahamia CCM



Na Wilhelm Mulinda, Mwanza

ALIYEKUWA mgombea ubunge Jimbo la Sumve, mkoani Mwanza, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Bw. Milton Rutabana, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza jana mbele
ya Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Deogratius Rutabana, alisema ameamua kukihama chama hicho kutokana
na matumizi mabaya ya ruzuku inayotolewa na Serikali.

“Sikuridhishwa kabisa na matumizi ya chama hiki ambacho kila mwezi kinapata ruzuku ya mamilioni ya fedha kutokana na wingi
wa wabunge wake lakini zinaishia tu Makao Makuu ya chama Dar es Salaam badala ya kwenda hadi ngazi za chini,” alisema.

Aliongeza kuwa, kitendo hicho ni sawa na kuwaibia wananchi kwani fedha hizo zinapaswa kutumika katika shughuli za maendeleo ya wananchi na kuendeleza chama katika ngazi mbalimbali nchi nzima.

Bw. Rutabana alisema CHADEMA kina matatizo katika mfumo wake wa uongozi ndio maana viongozi wake wa kitaifa wamekuwa wakijichukulia uamuzi bila kuhusisha ngazi za chini.


“Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, mapema mwaka huu aliwavua uanachama madiwani wawili Bw. Henry Matata wa Kata ya Kitangiri na Bw. Adam Chagulani wa Kata
ya Igoma jijini hapa bila kuhusisha vikao vya chama katika
ngazi husika,” alisema Bw. Rutabana.

Alisema hali hiyo inaonesha ni jinsi gani chama hicho kisivyo
na viongozi wanaostahili kupewa nafasi ya kushika dola kwani wanaweza kuleta matatizo kutokana na uroho wa madaraka.

Alisema kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Willbrod Slaa kumiliki kadi mbili za vyama tofauti vya siasa moja ya CCM na CHADEMA, kinaonesha viongozi wa chama hicho ni mamluki na kwamba kasoro hizo zinatosha kumfanya ajiondoe.

4 comments:

  1. uko alikokwenda ndicho chama kinachopeleka fedha kwenye matawi?,mbona waandishi wetu amuulizi hao watu wanapokuwa wanatangaza huo ujinga wao?.ccm matawi na kata hayapati ruzuku ingawa wanamiradi na fedha kibao hadi ngazi ya kata na ruzuku zaidi ya 1.5bilion.nafuu virus hivyo vijondoe mapema kuacha mimea ikue yenyewe

    ReplyDelete
  2. wale wote wanaojiunga na vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi binafsi watahamahama hadi wamalize vyama. Zama hizi watanzania wanatafuta maendeleo na siyo blaa blaa. nawasihi viongozi wa vyama vyote vya siasa wakiona yeyote anayehamia huko kaletwa na tumbo lake wamtimue ili hatimaye kiongozi kama huyo arudi kukaa nyumbani na mkewe na atoke kwenye siasa za zama hizi za kuongeza kasi ya maendeleo.

    ReplyDelete
  3. HONGERA KWA KUONDOKA NA SERA YA CHADEMA NI KWAMBA HATULIPANI POSHO. NA WEWE UNATAKA POSHO,UMEFANYA UAMUZI WA BUSARA HUKO ULIKOENDA CCM ZIKIINGIA TU UTACHUKUA KIASI CHAKO ZINAZOBAKI UTPELEKA MAKAO MAKUU.WEWE NI MMOJA WA MAKAPI ONDOKA CHAMA KIJENGEKE NA VIONGOZI CDM MSITIKISIKE KWA YOTE HAYA NI MAPITO YATAPITA TU.BAADA YA DHAMIRA YAO KUSHINWA 2015 NCHI YETU KUMBUKENI AHADI ZENU KWA WANANCHI. MUNGU AWE NANYI.AMINA

    ReplyDelete
  4. Njaa mbaya bwana haya wewe safari njema,huko utaridhika na matumizi ya ruzuku

    ReplyDelete