28 December 2012
Mgogoro wa Mulugo, Sugu washika kasi
Na Mariam Mziwanda
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo.
Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Majira kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim.
Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye
ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma.
“Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda
mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo
yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano
na yeye,” alisema Bw. Mulugo.
Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari
na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma.
Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la.
Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi.
“Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema.
Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja
na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani.
“Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi, ajifunze ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu
bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema.
Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa.
Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu viziri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe
kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima.
Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana
muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi.
Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni wazi Mulugo atakuwa na matatizo katika elimu yake,hata kama anajina la ukoo lakini jina aliloandikishwa kuanzia shule ya msingi ndilo uwa linatumika hadi elimu ya sekondari na kazini pia, je kama yeye sasa anaitwa Philipo Mulugo, jina la AMIM limefia wapi?, pengine angeendelea klitumia jina ilo la AMIM na kuitwa Philip Amim Mulugo lingeleta sense na katika mazingira ya kawaida tu something fishy somewhere.MULUGO ANAKESI YA KUJIBU NA ASIMTISHE SUGU KWA JAMBO LOLOTE HATA SISI TULIOSOMA KUNA VITU SIYO VIZURI TULIFANYA ENZI HIZO ,KAMA KUIBUA WALI NA MAHARAGE JIKONI NA IMEBAKI HISTORIA
ReplyDeleteyaaaaaap. "ur suppose to use the name that appear in ur form 4 academic certificate" hiyo n conditionalitz za form za body ya mkopo na vyuo vikuu sasa huyo amim asizan ss n viraza like him we know each & everthngs lazma ajibu hoja hiyo.
Deletenawe una tatizo sijui elimu yako . LAKINI MAWAZO YAKO YAMEHARIBIWA NA KIZUNGU CHAKO, SIO KILA ANAYEJUA JAMBO NZURI ASEME KIZUNGU, MBONA WACHINA WAKO MBALI NA WENGI WAO HAWAJUI LUNGA HIYO UNAYOLAZIMISHA WEWE ILI UONEKANE NAWE UMESOMA
Deletehuyu mbunge si ndio yule alisema ni muungano wa tanganyika na zimbabwe??????!!!!kuna kitu hapo si ajabu kwelikagushi huyo...
ReplyDeleteKwanini jina la ukoo liwe na mantiki baada ya kufika eliimu ya juu? danganya toto....... thibitisha kama uliapa mahakamani kuwa tangu wakati huo utaitwa philipo kama mbadala wa Amim hiyo haitoshi bila kueleza kwa undani sababu hasa ya kubadili jina, kama ulirudia darasa la saba ni vemna lakini kwanini hukuomba kubadili pindi ulipo kuwa sekondary maana utaratibu huwa kabla huja sajiliwa kufanya mtihani wa kidatocha pili hutolewa muda wa kufanya hivyo.
ReplyDeletendiyo maana kuna walimu wengi wenye vyeti feki na wenye vyeti vya watu wengine wenye majina ya kuunga kama yake ndiyo maana anashindwa kuwachukulia hatua. mimi ni mfanyakazi wa Halmashauri ya Mvomero nina walimu wawili wanatumia majina yaliyotumika na mmoja wao 1999 kigurunyembe Sekondari (Maria Zacharia James na Maria Zacharia Ally) hao walisoma pamoja na mmoja (Ally) alipata Div. 0 na James alipata Div III, mulugo tumemwambia lakini kashindwa kuchukua hatua, kumbe hachukui hatua kwa sababu na yeye ana tatizo hilo?
ReplyDeleteNDIO MAANA KIWANGO CHA KUFAULU KINASHUKA HATUJUI NI KWANINI??? WAZIRI ANA ELIMU YA KUUNGA UNGA ...BASI WIZARA NZIMA ELIMU YA KUUNGAUNGA
ReplyDeleteKama alisema Tanzania ni muungano Tanganyika na Zimbabwe unategemea nini hapo, tena ni waziri. Ingekuwa kwa wenzetu wa Ulaya angejiuzuru. Tuangalie nafasi yake ya uwaziri kaipataje. Bosi wake alitumia vigezo gani kumteuwa kuwa naibu waziri.
ReplyDeleteHII SASA INAONYESHA DHAHILI JINSI ELIMU YA VIONGOZI WENGI ILIVYO YA KUUNGA UNGA NA HIVYO RAIS KUFANYA UTEUZI KUFUATA KUMBUKUMBU ZA KUUNGA UNGA ZILIZOPO.
ReplyDeleteNADHANI SASA HILI LIWE SOMO KWA TEUZI NA ELIMU YA WATEULIWAJI IDHIBITISHWE NA MAMLAKA HUSIKA KAMA MOJA YA VIGEZO VYA KUMTEUA MTU KATIKA NAFASI FULANI.
HII YA 'MAUGO'INASIKITISHA SANA WANANCHI HATUMUELEWI NA SWALA LA KUITISHA MKUTANO WA WAANDISHI SI HOJA ATHIBITISHE KWA KUJIBU HOJA YEYE MWENYEWE KWA KUSCAN VYETI VYAKE VYOTE AVIWEKE GAZETINI TUVIHAKIKI ASIFANYE MCHEZO NA MAMBO YA VYETI.MHE.THIBITISHA ACHA LONGO LONGO.
HAYO NI MAWAZO FINYU YA KIZAZI CHA LEO HAWANA ADABU IKUMBUKWE WAKATI WA AWAMU ZA NYUMA HAPAKUWA NA FURSA YA KWENDA CHUO KIKUU DIRECT UNAPOMALIZA FORM SIX ILIBIDI UTOKEE KWENYE AJIRA NDIO UENDE CHUO KIKUU ,KWENDA CHUO KIKUU DIRECT ILIRUDISHWA ILI KUWASAIDIA WANAWAKE ILI KUBALANCE GENDER SASA KWA KUWA WASOMI WA DOTCOM WANAJIDAI WAMESOMA SANA MBONA BADO TANZANIA INAENDELEA KUWA SOKO LA BIDHAA TOKA ULAYA ,MBONA BADO TANZANIA NI SHAMBA LA MALIGHAFI YA VIWANDA VYA ULAYA KAMA ENZI ZA UKOLONI HIVI ELIMU YENU INA TOFAUTI IPI NA ILE YA MKOLONI SI AJABU YA MKOLONI AU BAADA YA UHURU ILIKUWA BORA ZAIDI KWANI WALIKATAA KUVUNA MADINI MPAKA KUANDAE RASILIMALIWATU SASA NDIO HAWA WANAENDELEA KUSISITIZA KUWA SOKO LA BIDHAA ZA VIWANDA VYA ULAYA AU KUENDELEA KULISHA VIWANDA VYA ULAYA NA MALI GHAFI KUTOKA TANZANIA KWELI NYINYI NI COPY AND PASTE HAKUNA UBISHI KUBWABWAJA TU
Deletehebu soma hii,In 1954, Julius Nyerere, a school teacher who was then one of only two Tanganyikans educated to university level, organized a political party—the Tanganyika African National Union (TANU). On December 9, 1961, Tanganika became an autonomous Commonwealth realm, and Nyerere became Prime Minister, under a new constitution. On December 9, 1962, a republican constitution was implemented with Mwalimu Julius Kambarage Nyerere as Tanganyika's first president.hii inamaanisha maendeleo hayaletwi na theoretical education.
Deletehttp://youtu.be/e3BNegmIUKM Angalieni huyo naibu waziri wenu aliyo yasema cape town... inasikitisha mtu hajui hata nchi yake anakuwajewaziri
ReplyDeleteSUGU UMESEMA VIZURI, JAMAA ANA ELIMU LAKINI NI YA KUUNGAUNGA (NIONGEZE KITU HAPA - KWA GUNDI). JAMANI HIYO HOTUBA YAKE KULE S.AFRIKA MMEIONA KWENYE YOUTUBE? KINGEREZA SI KINGEREZA (NAFIKIRI NI KINGREDHA) NI AIBU. KWELI HATA KAMA ULIMI ULITELEZA, TANZANIA ITAKUWAJE MUUNGANO WA PEMBA NA ZIMBABWE! ANA BAHATI MUGABE HAKUWEPO, ANGEMTIA ADABU.
ReplyDeleteni nafiri jambo la kujadiri ni namna mtu anavyo weza kutumikia nafasi yake aliyopewa kufanya kazi kama mtendaji wa umma kwa wananchi , na wala si wapi katokea na jina gani analotumia kwan hawa ambao wanamajina ya kuunga unga hawa na mchango katika maendeleo ya nchi bro sugu na wenzio ndio mmetoa asilimia mia za maendeleo hapa nchi lazima tutambua wajibu wa kila mtanzania katika nnchi yetu na tuweze kuwatumia ipasavyo ,sitaki kuhukumu moja kwa moja ebu tujiulize kila mmoja alipotoka mpaka alipo sasa elimu aliyokuwa nayo aijarishi kaitoa wapi imeleta tija kwa maendeleo ya nnchi .jamani tusiwe watumwa wa siasa ebu tuwe watumwa wa maendeleo
ReplyDeleteIli uwe kiongozi safi ni lazima uwe mkweli,kushindwa kuwa mkweli hata kama ungekua na elimu safi sana sifa kubwa umeipoteza. Mhe sifa zote yaelekea hana maana hata mwenyewe kashindwa kuwaeleza hao waandishi kitu cha kueleweka na bahati mbaya waandishi wetu wakashindwa kuomba ufafanuzi mzuri, labda kama waliitwa kumsafisha bado na wenyewe hawakumsaidia. I know how much is expensive to be honest especially to most of my fellow Tz who never take thier time to reason and give answers in a logical manner
DeleteNini kiingereza bwana, ile lafudhi tu ilikuwa ni kichekesho ile mbaya!!! Kinyakyusa si kinyakyusa, kisafwa si kisafwa, kinyiha si kinyiha duuuu!!! ilikuwa balaa!!!!
ReplyDeleteNAMSHUKURU SUGU KWA KUWEKA MAMBO HADHARANI MIMI KAMA MMOJA WA WAHITIMU WA MBEYA DAY MWAKA 1996. NAKUMBUKA NIKIWA KIDATO CHA KWANZA MLUGO ALIKUWA MBELE YANGU AKIJULIKANA KWA JINA LA AMIM NA ALIPOMALIZA KIDATO CHA NNE ALIENDA SONGEA BOYS ALIPOTOKA HUKO NA KUANZA KUFUNDISHA SHULE YA SEKONARI SOUTHERN HIGHLAND WAKATI HUO IKIMILIKIWA NA MUHINDI ALIJULIKANA KWA JINA LA MULUNGU ALIPOMALIZA OPEN KAIBUKA NA JINA LA MULOGO. MBONA ANATUCHANGANYA?MBONA HAJAELEZA ILI JINA LA MULUNGU ALILITOA WAPI? AU ANATAKA TUMUELEZE MWENYE JINA HILI YUKO WAPI?NAKUSHAURI NAIBU WAZIRI UKAE KIMYA KWENYE MASWALA YA ELIMU TUNAUCHUNGU SANA SISI TUNAOKUFAHAMU KUONA WEWE NI WAZIRI NA ELIMU YAKO YA KUBADILI MAJINA. NAAMINI MIAKA MICHACHE IJAYO UTAIBUKA NA MASTERS NA JINA JIPYA. UTAKAPO KUWA UNATHIBITISHA ELIMU YAKO UUELEZE UMMA WA WATANZANIA KIINI CHA WEWE KUITWA HAMIM PALE MBEYA DAY HADI SONGEA BOYS KISHA MULUNGU PALE SOUTHERN HIGHLAND SEKONDARI NA HILO LA MULUGO BAADA YA KUMALIZA OPEN.KWA MWENENDO HUU KWA NINI WATANZANIA WASISEME ELIMU YAKO NI YA KUUNGAUNGA. KAA KIMYA KAKA MSHUKURU MUNGU KAKUPA UNAIBU WAZIRI KIMIUJIZA, KIELIMU UWEZO WAKO NI MDOGO NA INATUUMA TUNAPOONA WADOGOZETU KAKAZETU NA WATANZANIA KWA UJUMLA WANAONGOZWA NA WATU WENYE AINA YAKO YA ELIMU.
ReplyDeleteNasikitika sana kwa wanaoona elimu ya kuunganisha si kitu Mulugo kaonyesha mfano kwa watu wengine, kuwa hata yatima anaweza kusoma. Nyie mliosoma naye Mbeya Day mnadai baada ya kumaliza form four alienda form six, sasa elimu ya kuunga kwa vipi? Mnadharau open university wakati kwa sasa ndo imeweza kuwafanya hata wasio na uwezo wasome.
DeleteHAAAAAAAAAAAAAAAAA! KWANZA HAMIM, PILI MULUNGU, TATU MULUGO, NNE..... KAKA LAZIMA TUWE NA SHAKA NA ELIMU YAKO.NAPATA HOFU NA ILI JINA LA MULUNGU KWANI KUNA JAMAA ALIMALIZA SONGEA BOYS AKAENDA MLIMANI NA SASA NI MHADHIRI MSAIDIZI MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION (MUCE)KWA SASA YUPO TENA MLIMANI ANASOMA PHD, ISIJE IKAWA MUHESHIMIWA ALITUMIA VYETI VYAKE?WATANZANIA NAOMBA TUSAIDIANE KUFUATILIA HILI ISIJEKUWA NAIBU WETU ALITUMIA VYETI VYA MULUNGU HUYU.MIMI NI MUHITIMU WA SONGEA BOYS, HUYU JAMAA MULUGO KWA SASA NILIKUWA NAFANANISHA SURA NA YULE AMIM NILIYEMUONA BOYS LAKINI JINA NDIO LILINICHANGANYA KABISA NIKAHISI NI MTU TOFAUTI NA KUAMINI KUWA DUNIANI WAWILIWAWILI NASHUKURU SUGU KWA KUTUFUMBUA MASIKIO. WATANZANIA WENZANGU TUSHIRIKIANE KUPATA UKWELI WA HILI, HIVI HAWA WASHAURI WA RAIS WALIMSHAURI KWELI KUMTEUA HUYU JAMAA KWA KUZINGATIA ELIMU YAKE AU SIASA?TUTAWEZAJE KUBORESHA ELIMU CHINI YA AKINA THREE IN ONE?HAMIM, MLUNGU, MULUGO WHY????????????
ReplyDeleteNIKWELI MHESHIMIWA MULUGO ELIMU YAKE NIYAKUUNGAUNGA KWA NINI ABADILISHE JINA NATUNA UHAKIKA GANI KAMA JINA HILO NILA UKOO KWELI KWA MAJINA MENGI YA UKOO HUWA YA NALANDANA NA KOO NYINGINE NASIKITIKA KUWA NA NAIBU WAZIRI WA ELIMU WA ANA KAMA YA MULUGO HII INADHIHIRISHA WAZI KWAMBAQ SI MULUGO TU WAPO MAWAZIRIWENGI NAMANAIBU WENGI KAMA MLUGO NDOMAANA WANAFANYA MAMBO SIYO
DeleteKWA DIZAINI YA ...... [CJUI nimite nn: AMIM, MULUNGU PHILIPO MULUGO] MIKATABA FEKI HAITAEPUKIKA. ALIYEMTEU AMUWAJIBISHE KWA KUMSHINIKIZA ATHIBITISHE MWENENDO WA ELIMU YAKE KWA UMMA WA WATZ. KUKAA KIMYA KWA ALIYEMTEUA KUNANIAMINISHA KUWA NAYE ANAMASLAHI NAYE UKIZINGATIA WANAACHWA WALIMU WAZAGAE KWA TAKRIBAN MWEZI WA 7 HUU- HII NDIYO IMEKUWA STAILI YAO TOKEA 2010.
ReplyDeleteMUITE, HAMIM AGUSTINO MULUNGU PHILIPO MULUGO HAYO YOTE NI MAJINA YAKE YAMETOKA WAPI ITABIDI ATUFAFANULIE.SINA UHAKIKA KAMA ASSIGNMENT ZA OPEN ALIKUWA ANAFANYA MWENYEWE...HII NDIYO TANZANIA YA WATANZANIA KUNA WATU WAMEPIGASHULE MPAKA NYWELE ZIMENYONYOKA LAKINI MAISHA YAO HOVYO WENGINE WAMEUNGA UNGA LEO MAWAZIRI?HALAFU TUNALALAMIKA SHULE ZA KATA HAZIFAULISHI TATIZOLETU WATANZANIA NI LA KIMFUMO KUANZIA IKULU, NASIKIA JAMAA HUYU ALISOMA NA ALIKUWA BEST FRIEND NA MTOTO MAARUFU WA MKUU WA KAYA KWAHIYO CHEO HICHO NI ZAWADI
DeleteKUONYESHA KUWA ANA UPEO MDOGO NDIYO MAANA KASHINDWA HATA KUJITETEA,ANAPOSEMA MLUGO NI JINA LA UKOO, KWANINI SHULENI HAKUITWA HAMIM PHILIPO MLUGO AKAITWA HAMIM AGUSTINO PALE MBEYA DAY?MBONA HILI JINA LA AUGUSTINO NALO HAJAELEZA LIMEFIA WAPI.USHAURI WA BURE KAMA ALIVYOSHAURI MTOA MAONI ALIYETANGULIA KAKA KAA KIMYA DUNIA YA SASA NI KIJIJI USIHANGAIKE HATA KWENDA KWENYE MIKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWANI WATU WANAONGEA KWA TAKWIMU SIKUHIZI KAKA. MI MWENYEWE BAHATI NZURI NINA VIDEO YA HOTUBA YA HUYU MUHESHIMIWA KULE SOUTH, SASA KAMA HOTUBA ILE ILIKUWA IMEANDIKWA KAZI YAKE ILIKUWA KUSOMA TU NA AKACHEMSHA YA KUANDAA MWENYEWE ITAKUWAJE?PICHA WALIYOPATA WAHUDHURIAJI WA MKUTANO ULE NI KUWA JAMAA NDIYO MIONGONI MWA VICHWA SAFI VYA TANZANIA MPAKA AKATUWAKILISHA KULE.HII NI AIBU NDUGU HAMIM AGUSTINO MULUNGU PHILIPO MULUGO.SHUKURU MUNGU KWA NAFASI HIYO WAPO MAPROFESSOR WAMEIKOSA.KULA KAKA HAYO NDIYO MATUNDA YA CCM TENA WEWE NI MJUMBE WA NEC BIG UP HAMIM AUGUSTINO MULUNGU PHILIPO MULUGO NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
ReplyDeleteElezeni nn mtawafanyia na mmewafanyia wananchi hayo ya elimu wengi waliounga.Mlituahidi ghorofa za Mbao miaka inaisha vp jamani.Kama elimu ndio utendaji hebu tuwalinganishe wale maprofesa na madokta na Hawa Vihiyo tuliowapeleka bungeni waliotufanyia zaidi ya kula posho tu
ReplyDeleteKaka wengi kuwa na elimu ya kuunga haimaanishi watu kutoongelea swala la elimu. Kubali kataa elimu ndiyo kila kitu we unafikiri umasikini huu wa watanzania uliletwa na mungu?Chano ndio hiki cha watu wenye elimu zao na fani zao kunyimwa nafasi ya kutumia taaluma zao na nafisi hizo kupewa vihiyo, matatizo yote ya nchi hii chanzo chake ni elimu, tumeingia mikataba mibovu kwa sababu ya elimu duni ya tuliowateua kutuwakilisha kwenye mikataba. Wakati wa UPE wanafunzi waliferi sana wasababu walimu walikuwa ni waliofeli sasa leo unafikiri tutaboresha elimu kwa kuwa na watu wenye elimu za kina MULUNGU HAMIM PHILIPO AGUSTINO MULUGO?FUMBUA MACHO KAKA HUWEZI KUONGELEA WANANCHI WAMEFANYIWA NINI BILA KUGUSA SWALA NYETI LA ELIMU HASA ZA WATU WANAOTUONGOZA
Deletetatizo ni elimu au jina?
ReplyDeleteMULUGO NA NCHEMBA WATUAMBIE WATANZANIA KUHUSU ELIMU ZAO
ReplyDeleteHii kweli vihiyo mpo wengi,wanaonyesha hawaelewi taratibu z majina ya watu, wanakurupuka tu, mmekuwa wanasiasa au mnaleta ushabiki, kama elimu ni ya kuunga mboa hasemi alipomaliza O-level matokeo yalikuwa Vipi,inamaana Sugu alifeli na Jamaa akapeta? sasa wivu wa nini? kusoma wote isiwe tatizo. Mbona hata yeye anaweza kusoma hata sasa? acheni hizo wivu tu, waulizeni aliosoma nao elimu ya Juu wanasema nini?
ReplyDeletewalimwengu wanishangaza, huyu ndg anayetetea udanganyifu, (nasema udanganyifu coz ameshindwa kudhibitisha)wa mhe.nae nina wasiwasi nae ana lake anficha ama uelewa wake unakaribiana na wa huyu jamaa. Huezi kuendesha wizara pasi kuwa interlectual utabaki kufanya maamuzi ovyo ama ya mtu mwingine. kisha wewe kama waziri wadanganya umma huoni kuwa uko tayari kuendelea kudanganya, kufanya vitu hata kama huelewi ili kuficha aibu, na tena kuendelea kuaibisha nchi duniani. Huyu anaemtetea Hamin Augustino Mulungu Philipo Mulugo pamoja na madudu anayoyafanya ??? IQ!!!
ReplyDeleteMuulizeni na Wilbroad Slaa hiyo PhD yake ya sheria za dini au ukipenda (Shariah)alipataje? Mbona hatuambiwi degree ya kwanza (bachelor) na degree ya pili (master) alisomea wapi na katika fani zipi? Huyu naye sio Kihiyo kweli? Si kwamba na yeye elimu yake ni ya KUUNGAUNGA kama ya mh. Mulugo ukipenda muite Hamim?
ReplyDeleteache marumbano watumikieni wanainchi kwenye majibo yenu msije mkakosa ubunge mwaka 2015 hata mimi ubunge nautaka
ReplyDeleteAcha waendelee kulumbana wakati ukweli upo uchi kabisa majimbo hayo tunayatamani so acha walumbane tupate pointi za kumwangusha aliye kilaza hapo ukweli hapo unafahamika zaidi na ni kwa viongozi wengi si hao walumbanao.
ReplyDeleteAh! HAMIM AUGUSTINO MULUNGU PHILLIPO MULUGO hii kali. Eti hilo la Mulungu alichakachua jina la Kindali kabila la Ileje. Alipotaka ubunge ndipo ikabidi jina liwe Mulugo la kabila ya Wabungu huko chunya.
ReplyDeleteMlugo yote hayo ya nini chapa kazi mzeeeeeee
ReplyDeleteDaaaa...!!!Kwajinsi ninavyokufaham Shakiru Bujugo toka tukiwa shule kamwe sikutegemea kama utakuja kuwa na akili za kipumbavu.Hiv suala la kushuka kiwang cha elimu unalichukulia pouwaaaaa!!!!DOGO ACHA USENGE KUMTETEA WAZIRI WAKO MSHENZI MULUGO.....KUDADADEKI MKUBWA......!!!!!!!!
DeleteLakini hili suala la mawaziri kudanganya kuhusu elimu walio nayo si la kubeza kwa sababu wanapewa nyadhifa ambazo hawana uwezo. Ndio maana Mwigulu Nchemba alivyoelezwa kuhusu hilo amekaa kimya mpaka leo. Mapepe yote yametulia kimya. Jina si lake analotumia jina lake halisi ni Lameck hatujui ni kwa nini anatumia jina si lake hawa magamba tuachane nayo wana ajenda yao ya siri.
ReplyDeleteMTUAMBIE NYIE AMBAO HAMKUSOMA ELIMU YA KUUNGAUNGA MMEIFANYIA NINI NCHI YETU.
ReplyDeleteFAINALI UCHAGUZI 2015 MAHAKIMU NI WAPIGA KURA
ReplyDeleteSUGU.....!!! heshima kwako mkuu.Suala la mulugu hata president wao analifaham fika.Hivi udokta kautoa wapi?WATANZANIA TUWE MACHO NA MAFISADI HAWA WATATUMALIZA...!!!!
ReplyDeleteunazi..
ReplyDeleteinaruhusiwa kuchange names..kuna form ya mahakama inaitwa ''deed pool..so is not a big deal.
ReplyDeletekama vipi hao wote wakutane na hvyo vyombe vya habari then ukweli uanikwe kama mmoja wao alvyoshauri..scientifically.
vema kujadili vitu vya msingi ZAIDI enyi wananch.linalohusu utendaji ni muafaka zaidi kuliko ubinafsi..acheni unazi na vyama vyenu,MNATUZINGUA!!!!
john heche wa cdm vyet vyake vya taaluma vmeandikwa wegesa suguta...very easier.
ReplyDeletekunawatu wanaitwa opportunist hawa huwa wako tayari kwa lolote,mara wanapoona fursa,sio jambo jipya
ReplyDeleteLAITI HUYO MULUGO ANGEKUWA MWISLAM UNGEWASIKIA WAPAYUKAJI MAASKOFI WAKIMBEZA LAKINI KWAKUWA WAO NDIO WALIOMTENGENEZEA HICHO CHETI NA KUCHUKUA JINA MWISLAM HAMIM NA KUTUMIKA KAMA MULUGO YANI AIBUUUUU SSSAANN MPAKA KICHEFUUUUUUUUUUUCHEFYAAA MH HILO NI ZAO KUTOKA SENT PAROKO.
ReplyDeletejamani inapobidi na kwa kulinda maslai ya chama lazima umuweke mtu mwenye uzalendo wa kweli kabisa katika nafasi kama ihi ya kuwatumikia wananchi hata kama kuna urakini wa vitu furani philiiiiipo aruta continiuaaaaaaa weweeeee wakikupa tena kandamiza mwanangu ,kufa kwaja
ReplyDeleteSi sawa kuwakatisha tamaa ya kusoma sasa wale wote waliokosa nafasi ya kusoma moja kwa moja, Elimu ya kuunga si dhambi na wala tusiibeze, ni njia sahihi ya kujiendeleza kielimu kwa walioikosa. Jadilini tofauti na mapungufu yenu sio mfumo halali wa elimu.
ReplyDeleteNdugu zangu..watanzania wenzangu,,wa afrika wenzangu haya tunayo yaona leo sio yameanza jana haya yaliasissiwa na Mwl NYERERE tunaye muita BABA WA TAIFA.... ni wapeni mfano mmoja...nendeni pale wozara ya elimu nje kwenye mbao za matangazo utaona list ya mawaziri na manaibu waziri wa elimu tangu wizara iundwe...kuna waziri mmoja alipewa nafasi sio kwa ajili ya elimu yake bali kwa ajili ya IMMANI YAKE THAABITI JUU YA DINI YAKE YA UKRISTO TENA MKATOLIKI KAMA RAISI ALIYE KUWA MADARAKANI NA HILI ALILITHIBITISHA MWL NYERERE MWENYEWE ALIP[O U;IZWA AKIWA ANALIPA FADHILA KWA KANISA KATOLILKI...NDUGU ZANGU HAPANA MAHALA AMBAPO WATANZANIA WANADHULUMIWA KAMA MNECTA NA WIZARA KWA UJUMLA,,,,MADUDU MATUPU NA HII NI KWASABABU WIZARA NA NECTA ZIMEKUWA PAROKIA KATOLIKI NCHINI NA HAKUNA ATAYEINGIA PALE ILA MTU WAO WALIO MUANDAA NA AWE TAYARI KUYATETEA MASLAHI YAO...TUJIULIZE KWANN KILA SIKU SHULE ZA MAKANISA ZATYESA????HASA KATOLIKI SCHOOLS??/RUZUKU WANAYOPEWA NA SERIKALI KUPITIA MOU ALIYOSAINI Mh.LOWASA 1992 NA CCT NA TEC NA MENGINE MENGI MACHAFU KANISA LINAYAFANYA KWA MASLAHI YAKE HATA KWA KUFANYA LOLOTE KWA AJILI YA MASLAHI YAO
ReplyDelete