20 December 2012

Kikosi cha Sauti Moja chaongeza wajumbe


Na Darlin Said

KIKOSI kazi cha Sauti Moja ya Sekta Binafsi nchini, kimeongeza wajumbe wanane na kufikia 18 badala ya 10 wa awali.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezeji), Dkt. Mary Nagu, aliyasema hayo Dar es Salaam juzi, katika Kikao cha Pili cha Uimarishaji na Uendelezaji Sekta Binafsi nchini.

Alisema ongezeko hilo la wajumbe litasaidia kupata sekta binafsi yenye nguvu ambayo itachochea maendeleo endelevu na ukuaji  uchumi hasa katika nyanja ya kuongeza ajira.

Wajumbe wapya ni Chama cha Wanasheria (TLS), Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), CEO Roundatable Tanzania na Chama cha Wafanyakazi Walemavu.

Wengine ni Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Association of Tanzania Insurers (ATI) na Chama cha Wenye Mabenki nchini (TBA).

Awali kikosi hicho kilikuwa kinaundwa na Mahakama ya Biashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA), Mashikamano juu ya Usafiri
na Kanuni za Biashara (TACO), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Taasisi ya Saratani ya Matiti (TNBC), Shirikisho la Viwanda nchini (CTI), TCT, TCME, TAFFA na VIBINDO.

Katika mkutano huo, Dkt. Nagu, aliwataka wajumbe hao kutumia muda wao kuangalia changamoto ambazo zinawakabili pamoja na kuondoa zilizobainika ndani ya sekta yao.

No comments:

Post a Comment