25 September 2012

Viongozi washauriwa kuwajibika ipasavyo


Na Zourha Malisa

WITO umetolewa kwa viongozi kuwajibika, kusimamia majukumu yao ipasavyo ili kuharakisha maendeleo ya jamii na Taifa.


Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathimini Kiutawala Bora (APRM) nchini Bi. Rehema Twalib, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema wameandaa mafunzo ya siku mbili ambayo yatafanyika leo na kesho kwa watendaji wa Serikalini na wadau mbalimbali ili kuoanisha mipango wa APRM Tanzania na mingine.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka ambao Tanzania na mataifa mengine ya Afrika yako katika kipindi muhimu cha kutafakari namna bora ya kutekeleza mipango yao.

“Hatua ambayo itafuata ni kukabidhi ripoti yenye mapendekezo ya nini Tanzania ifanye itakayowasilishwa Oktoba mwaka huu ambapo Januari 2013, Rais Jakaya Kikwete ataiwasilisha nchini Ethiopia na kujadiliwa mbele ya wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU), ambazo zinashiriki katika mpango wa APRM.

APRM ni mchakato wa kujifanyia tathmini za utawala bora kwa kukusanya maoni ya wananchi.


No comments:

Post a Comment