29 August 2012

Ghana, Niger mabingwa Rising Stars



NAIROBI, Kenya

FAINALI za michuano ya Airtel Rising Stars Afrika, zimefikia mwisho huku timu ya wavulana ya Niger na wasichana kutoka Ghana, zikinyakua ubigwa.


Katika mechi hizo za fainali kwa upende wa wavulana, Niger iliifunga Zambia kwa mikwaju ya penalti 5-4 na kutangazwa mabingwa wa Airtel Rising Stars 2012.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa suluhu ndipo ilipolazimika mwamuzi kuongeza dakika 30.

Lakini ya kuongezewa dakika timu hizo zilishindwa kutambiana na kumaliza mchezo zikiwa hazijafungana na mwamuzi kutumia sheria ya kupigiana penalti tano tano kila upande.

Katika hatua za mikwaju ya penalti Niger walipata penati zote tano kupitia kwa Mamane Karibou, Issa Souleymane, Abubacar Timbo, Idrissa Amadou na Issifou Garba.

Kwa uipande wa Zambia waliofunga walikuwa Timothy Sakala, Thomas Juma Mutale, Dennis Chebuye na Albert Bwalya huku Shadrack Chimanya akikosa.

Kwa upande wa wanawake, Ghana walitoka nyuma na kuwafunga wenyeji Kenya waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda kwa mabao 2-1.

Kenya ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Vivian Odhiambo, dakika ya 27 kabla ya Emelia Lokko kusawazisha dakika ya 43. Patience Narh ndio alipeleka kilio kwa Wakenya kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 56.

Fainali hizo zilihudhuriwa na nyota wa zamani wa Manchester United, Peter Schmeichel ambaye pia amechanguliwa kuwa balozi wa klabu hiyo hivi karibu. Schmeichel ndiye aliyekabidhi medali kwa washindi.

Timu za Niger na Ghana zilizawadiwa fedha taslimu dola za Marekani 10,000 kila moja kwa kuwa mabingwa.

Pia timu hizo zitapata fursa kwa wachezaji wake wote kushiriki kliniki maalumu chini ya makocha wa soka kutoka Klabu za Arsenal na Manchester United za nchini Uingereza. Kliniki hiyo itafanyika Nairobi, Kenya na Accra, Ghana.
   

No comments:

Post a Comment