05 July 2012

Kamati UNESCO yaridhia Tanzania kurekebisha mpaka pori la Serious


Na Mariam Mziwanda

KAMATI ya Urithi wa Dunia, imekubali ombi la Serikali ya Tanzania ya kurekebisha mpaka wa Pori la Akiba la Serious.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyasema hayo Dar es Salaam jana na kufafanua kuwa, kamati hiyo ambayo inaendelea na kikao chake cha 36 nchini Urusi, imekubali ombi la Tanzania kurekebisha mipaka hiyo.


“Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), ambayo kamati yake imekubali ombi letu ili kutatoa fursa ya kuruhusu uchumbaji madini ya urani.

“Ombi letu lilipelekwa katika kamati hii kwa mara ya kwanza Januari 2011 na kujadiliwa katika kikao cha 35 lakini walifikia makubaliano ya kuendelea kulijadili katika kikao hiki cha 36.

“Kimsingi tumepambana ili kuhakikisha mjadala huu unamalizika salama ili kutoa fursa ya kuruhusu uchumbaji wa madini haya,” alisema Balozi Kagasheki.

Alisema kupatikana kwa kibari hicho, kutaiwezesha Tanzania kutimiza malengo yake kiuchumi na kijamii ambapo eneo lililokuwa likijadiliwa lina ukubwa wa kilometa 200.

“Makubaliano ya Serikali na wataalamu wanaochimba madini haya, hakuna athari zozote zinazoweza kutokea katika pori hili, Kamati husika imeitaka Serikali ya Tanzania, kuhakikisha kampuni ambayo itashinda tenda ya kuchimba urani ilipe fidia kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Serious na kusaidia wananchi waishio maeneo jirani ili waweze kunufaika na uchimbaji huu pamoja na kutoa ajira,” alisema Balozi Kagasheki.

Poli la Akiba la Serious lina ukubwa wa kilometa za mraba 50,000 pia ni moja ya hifadhi kubwa duniani zenye viumbe mbalimbali, eneo la nyanda kubwa tambarare zenye nyasi, misitu ya miombo na wanyama pori wa aina tofauti.

No comments:

Post a Comment