11 May 2012
Kesi ya Liyumba yaahirishwa
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kupatikana na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Bw. Amatus Liyumba, kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.
Wakili wa Serikali Bi.Elizabert Kaganda, alisema jana mbele ya hakimu Bi.Devota Kisoka, wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo. Alisema Bw.Suwart Sanga anaumwa hivyo ameshindwa kufika mahakamani.
Kutokana na hali hiyo kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Julai 2, mwaka huu. Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa, Julai 27, mwaka jana, Bw.Liyumba akiwa mfungwa kwenye gereza la Ukonga anadaiwa kukutwa na kifaa kilichozuiliwa kisheria ambacho ni simu aina ya Nokia, rangi nyeusi yenye laini namba 0653004662 na IMEI 356273/04/276170/3.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment