19 March 2012

Slaa afunika

  • Apokewa kifalme, aanza kwa kumvaa Wassira
  • Nassari aahidi kumwoa Mdee, Lema anguruma
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa, aliyeshika kipaza sauti akihutubia wakazi wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la akeri. Kulia kwake ni mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho Bw. Joshua Nassari. (Picha na Queen Lema)

wa kampeni uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu. Akihutubia mkutano , Dkt. Slaa alianza kwa kujibu mapigo yaliyoelekezwa kwake na Mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Bw. Stephen Wassira, aliyemtuhumu
kuwa alifukuzwa upadri baada kutafuna fedha za ujio wa Papa John Paul II kwenye miaka ya tisini. Huku akishangiliwa na wananchi,
 Dkt. Slaa alimtaka Rais Jakaya Kikwete, kumfukuza kazi Bw. Wassira kwa sababu ni waziri anayesema uongo, hivyo hafai kuongoza wananchi. “Wa s s i r a a k iwa wa z i r i amewadanganya wananchi kuwa nilifukuzwa upadri kwa sababu ya kula fedha...kiongozi wa aina hii hafai, kwani ni muongo na kama ana....basi ajiuzulu,” alisema Dkt. Slaa. Alisema Bw. Wassira anatakiwa kujua kuwa yeye (Dkt. Slaa) si saizi yake, kwani yeye ni namba nyingine tofauti na kumtaka aende mahakamani kama ana ushahidi na hilo. “Asipoenda mahakamani itakuwa inadhihirisha kuwa yeye ni muongo wa kutupwa na hafai kuwa kiongozi,” alisema. Kuhusu ubadhirifu wa fedha, alisema aligundua kuwa kwenye Halmashauri za Arusha Mjini na Meru kuna ubadhirifu mkubwa alioubani wakati akiwa mbunge.
Aliahidi kufichua uozo wote sehemu atakazopita. Alisema kwa sasa chama chake kimebadili muundo wa uongozi, hakishughuliki na wabunge wanaoenda bungeni kupiga makofi, badala yake wanataka ambao wanaweza kutetea maslahi ya wananchi. Alisema kwa stahili hiyo kamwe CCM haiwezi kuwakamata. Kwa upande wake mgombea ubunge, Bw. Joshua Nassari, naye alimvaa Bw. Wassira kwa kauli yake ya kutaka wananchi wasimchague kwa kuwa hajaoa. “Kwa kuwa wameniambia sijaoa, nitamuoa Halima Mdee (mbunge wa Jimbo la Kawe) ili wananchi wa jimbo hili wanufaike mara mbili, hivyo jimbo litakuwa na wabunge wawili,” alisema. Alisema anaomba Mungu usiku na mchana ili afanikiwe kumuona, Bi. Halima Mdee, ili akishinda ubunge wananchi wa Arumeru wawe na wabunge wawili, ambao watakuwa mke na mume.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, amemtaka mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, asithubutu kutia mguu Arumeru kwa madai atachangia amani kuvunjika. CCM, CHADEMA wazipiga Naye mwandishi wetu Pamela Mollel anaripoti kuwa, wafuasi wa vyama vya CHADEMA na CCM wameshambuliana katika tukio lililotokea eneo la Usariver baada ya kukutana wakiwa wamevalia sare za vyama vyao.
 Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni wakati kundi la wafuasi wa CHADEMA lilipokutana na mwendesha bodaboda akiwa amevaa nguo zenye rangi inayotumiwa na CCM na kuanza kushambuliana. Mara baada ya purukushani hiyo wafuasi wa CHADEMA walitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Arumeru wakilalamikia kufanyiwa vurugu. Taarifa za tukio hilo zilipowafikia wanachama wa CCM waliokuwa eneo lingine katika kata hiyo ya Usariver, akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM, Bw. Mathini Shigela, walienda Kituo cha Polisi Usariver na kusuluhisha sakata hilo. Mara baada majadiliano ya muda mrefu na jeshi la polisi, wana-CCM walikubali kuondoka na kuendelea na mikutano yao katika Kata ya Kikatiti.
 Mgombea CCM Wakati huo huo mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Bw. Sioi Sumari, ameahidi wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki kuhakikisha mradi mkubwa wa umeme unafika katika maeneo ambayo hayana nishati hiyo. Akihutubia maelfu ya wakazi wa Kata ya Maroroni katika mkutano wa hadhara wa kampeni za chama hicho, Bw. Sioi alisema atahakikisha maeneo ambayo hayana umeme yanapata huduma hiyo. Alisema katika kata hiyo kuna changamoto kubwa ya umeme, lakini amewatoa hofu wakazi hao kwa kuwa tayari kuna mradi mkubwa wa umeme ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni na tayari Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja, alishatembelea eneo hilo. “Wananchi ninawaomba mnipe ridhaa ili niweze kusimamia vizuri mradi huu kwa kuwa utaanzia huku na tayari tathimini ilishafanyika sasa kilichobaki ni ufuatiliaji ili kuhakikisha umeme unawafikia mapema,”alisema.
 Pia aliongeza kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni la kutafutiwa ufumbuzi mapema. Aliongeza kuwa kuna ahadi nyingi ambazo ziliahidiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Jeremia Sumari, ambazo bado alikuwa hajatekeleza.Kesi

12 comments:

  1. Acha niwambie Lowasa hana ubavu na Dr Slaa na Lema.Viongozi wa ccm wana sema mambo ambayo yalishawashinda.Iweje Dr Slaa awe mwizi Serikali ya ccm ndo iko madarakani kw3a nini wasimkamate???Je walionunua Rada wamekamatwa??Wa Buzwagi wamekamatwa,Dohansi je,EpA je.Au wanadhani watanzania wa leo ndo wa enzi hizo ???pole sana Wasira na serikali yako.Enzi ya Nyerere wala asingethubutu kusema uongo angevuliwa uongozi mara hiyo hiyo.Lakini Baba Riz ni sawa tu kwake. Ahsante.Ccm mnalo mmeshalivaa.Kulitegua ni ngumu wananchi wanasubiri tu uchaguzi hapa Arumeru,ccm waone kitakachotokea.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Mimi ninashangaa sana, ni LINI VIONGOZI WA CCM WAMEKUWA WASEMAJI WA FAMILIA ZA WANACHAMA WA CHADEMA! alianza Mkapa kala kapa, kaumbuliwa, sasa kaja Wasira na uongo mwingine kaumbuliwa na baba yake mzazi, taifa hili lina viongozi wa aina gaini? kwanini wasiongee issues badala ya watu binafsi?

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji wa kwanza na wa pili amenikuna panapo.Big up.Huo ndo ukweli.CCM ilishashindwa kuiongoza Tanzania.Naomba tuwape ridhaa CHADEMA.kwa mtazamo wangu nchi itaingia kwenye Neema lakini tukiendelea na CCM tumekwisha.Enyi wananchi wa Arumeru fanyeni maamuzi sahihi tuikomboe nchi yetu!!!

    ReplyDelete
  4. Kusema kweli tusiwalaamu CCM,KWA SASA HAKUNA KINGINE AMBACHO WANAWEZA kuwaambia wananchi zaidi ya kuwaambia uongo.

    ReplyDelete
  5. Binafsi nawalaumu sana wanasiasa wote wanaopiga kampeni huko meru kwa kuwataja watu badala ya kuelezea sera za vyama vyao na jinsi watakavyotumia sera hizo ktk kutatua matatizo ya msingi ya wananchi wa arumeru mashariki kama vile tatizo la maji, ajira kwa vijana,afya,elimu nk nk. Wanahangaika kuchafua watu wengine kifupi ni kwamba wamefilisika na ni wepesi sana kisiasa!

    ReplyDelete
  6. wasomaji kibaraka mwingine wa ccm ni blog ya HAKINGOWI muogopeni kama ukoma njaa inamsumbua hana cha zaidi kuibeba ccm tu

    ReplyDelete
  7. Watu wa kushindwa wanaeleweka tu. Hivi mnadhani huyo Wassira alifanya kama bahati mbaya kumchokoza Rais wetu wa Ukweli? ni mipango ya thithiemu (chama cha mafisadi)kutaka kumfananisha na wao, mi naomba waTz tukomae na mabadiliko tuachane na watu aina ya Wassira (Nyara ya Taifa kwanza alitakiwa kutunzwa katika nyumba ya makumbusho aje kuwa kumbukumbu ya Taifa letu tuongeze na mapato au hamuoni picha yake? si anafaa kuwa kivutio kimoja wapo nchini eee

    ReplyDelete
  8. Big Up no 1&2

    sisiem wameinama wameinuka wanaona...hao
    Wasira ungekua na mtoto wa kike bomba ningemuoa mimi

    ReplyDelete
  9. Lazima tubadilike jamani...na tuanzie huu uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki....CCM wale wale na ahadi zao zile zile ambazo mara nyingi zinakuwa hewa...Kwa stahili hii TZ hatutafika...CCM ni wa kuwaondosha kabisa madarakani ili nchi isonge mbele....Wameshindwa kazi waliyopewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ufisadi uko katika damu ya Watanzania wengi, isipokuwa hawana nafasi ya kufanya hivyo.. leo hii ni mfanyakazi gani anayeishi kwa jasho lake kila mwezi, wengi wanaiba, hata wafanyabiashara wanawaibia wateja na Serikali. Slaa pia ni fisadi unajua analipwa shilingi ngapi? na katibu wa Chadema wilaya alipwa shilingi ngapi? wanasiasa wote wanatafuta nafasi ya kula kama ilivyo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara, na hata wakulima nao wakipata nafasi ya kudanganya uzito wa mazao yao watafanya hivyo hivyo.....

      Delete
  10. Wote hapo juu ni vibaraka wa Chadema, ama kwa hakika wote mna njaa na labda chadema inawapa posho.
    Siasa siasa ibaki kuwa siasa....ndo mana Slaa hakujibu hoja ya Wasira badala yake akasema aende mahakamani kwani Wasira amekuwa kanisa katoliki?Kueonyesha kuwa ni vibaraka lolote analosema Slaa mnaunga mkono hata kama ni pumba...huu ni upuuzi kabisa. Kimsingi Slaa hana uwezo wa kuwa Rais, labda awe meneja wa propaganda.

    ReplyDelete
  11. Mtanzania amka.CCM imetunyonya damu,maji yaliyokuwa mwilini na sasa wanataka kunyonya mavi yaliyomo tumboni na bado umelala usingizi tuu.ni mtu wa namna gani wewe usiyeona?mbona hata wasioona(vipofu
    )wameamka?Acha kushabikia vyama,kinachotakiwa ni maendeleo.maendeleo yataletwa na wewe mwenyewe.acha kung'ang'ania ccm iliyooza.AMKA!AMKA!AMKA!.

    ReplyDelete