Katika taarifa iliyotumwa kwa Shirika la Habari la Ufaransa, AFP mjini Beirut, kundi la upinzani linalojiita Baraza la Taifa la Syria, liliiomba Jamii ya Kimataifa ichukue hatua na kuitaka Urusi ibadili msimamo wake, katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuulaani utawala wa Rais Assad, pamoja na kumshinikiza kiongozi huyo kuruhusu demokrasia.
Taarifa zinasema wanajeshi wa Syria walishambulia kwa makombora maeneo kadhaa ya raia, mjini Homs ikiwa ni pamoja na Wilaya za Khaldiyeh na Qusur na miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto.
Wanaharakati wanaopinga serikali ya Syria wamesema shambulio la jeshi dhidi ya mji wa Homs, limeuwa zaidi ya watu 200. Taarifa zinazohusiana Mashariki ya kati, ghasia wakazi wa mji wanaeleza kuwa mtaa wa Khaldiyeh ulishambuliwa kwa mizinga mingi.
Ikiwa watu 200 watathibitishwa kuuawa, basi itakuwa idadi kubwa kabisa kutokea katika siku moja tangu ghasia kuanza nchini Syria miezi 11 iliyopita.
Serikali ya Syria imekanusha kushambulia kwa mabomu eneo la Homs.Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema itakuwa aibu iwapo muswada wa azimio la Umoja wa Mataifa linalolaani matumizi ya nguvu yanayofanywa serikali ya Syria, lingepitishwa jana.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walitarajiwa kujadili muswada huo, ambao unaunga mkono mpango wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, kumtaka Rais wa Syria, Bashar al-Assad, akabidhi madaraka kwa naibu wake.
Bw. Lavrov alisema maneno yaliyotumiwa kwenye muswada huo, hayaridhishi nchi yake.
Urusi imesema azimio hilo lisitumike kuhalalisha jeshi la kigeni kuingilia kati Syria, pamoja na kupinga suala la kuwekewa vikwazo vya silaha.
Syria moja kati ya wateja wakubwa wa silaha za Urusi.Pardeftab720\sl320\sa260\ql\qnatural Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle, amelaani ukandamizaji wa utawala wa Syria, dhidi ya raia nchini humo na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuulaani utawala huo, katika azimio kali dhidi ya serikali ya Syria.
Katika taarifa yake nje ya mkutano wa Usalama mjini Munich, Ujerumani, Westerwelle alisema ripoti za kuhuzunisha kutoka mjini Homs, zinaonesha utawala wa Assad hauko tayari kusitisha matumizi ya nguvu.
BBC/DW}

No comments:
Post a Comment