24 January 2012

Migogoro ya ardhi inaweza kuepukika

Na Rachel Balama

ARDHI ni rasilimali ya msingi katika uhai wa maendeleo ya binadamu, wanyama, mimea na viumbe vyote. Nchi ya Tanzania ambayo uchumi wake unategemea kilimo kama sekta muhimu kukidhi mahitaji ya wananchi walio wengi.

Ardhi inakuwa rasilimali muhimu ambayo kila mwananchi hana budi kuipata na kuimiliki, kuitumia na kuitunza.

Ardhi ni rasilimali inayohitajika ili kuendeleza sekta nyingine za uchumi, ikiwepo viwanda, biashara, pia makazi ya binadamu ambayo hutegemea ardhi kwa ujenzi wa nyumba, barabara na matumizi mengineyo.

Hivyo basi ardhi ni haki ya kila binadamu na kumnyima mtu yeyote haki ya kuitunza, kuitumia na kuimiliki ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Kwa muda mrefu sasa mila na desturi nyingi katika nchi yetu zimekuwa  zinamnyima mwanamke haki.

Kabla ya Sheria mpya ya ardhi ya mwaka 1999 kutungwa, Sheria iliyokuwepo na. 113 ilionekana kuwa na mapungufu mengi suala lililopelekea kuundwa kwa Sheria mpya.

Kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye sheria hiyo  Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitunga Sheria mbili kuu za ardhi.

Sheria hizo ni Sheria ya ardhi na. 4 ya mwaka 1999, na Sheria ya Vijiji na. 5 ya mwaka 1999, Sheria hizi zimetungwa kuboresha mapungufu ya Sheria ya ardhi ya zamani ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Mwaka 2002 Bunge lilitunga Sheria nyingine iliyoanzisha mahakama za kutatua migogoro ya ardhi na. 2 ya mwaka 2002 ni Baraza la kijiji la Ardhi, Baraza la kata, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, Mahakama kuu (idara ya Ardhi) na Mahakama kuu ya rufaa ya Tanzania.

Japo kumekuwepo na sheria za ardhi lakini migogoro ya ardhi imekuwa kijitokeza kila kukicha na tawkimu zinaonyesha kwamba kwa siku kumekuwa na  migogoro ya ardhi isiyozidi 5-6.

Migogoro mingi ya ardhi inaletwa na sheria mama ambayo inamruhusu rais kuwa na mamlaka makubwa ya kuchukua rais, pia inamruhusu rais kuwekeza hilo ni tatizo.

Nini kifanyike,Uandaaji wa ramani ya mipango bora ya mipango miji na matumizi ya ardhi, kuwepo na usimamizi, sheria za ardhi zifanyiwe marekebisho.

Sheria ya madini ya mwaka 1999 inatakiwa ifanyiwe marekebisho kwa kuwa kuna kipengele kina tamka kwamba eneo la madini si sehemu ya ardhi kwani hilo ni tatizo.

Halmashauri zipunguziwe majukumu kwa kuwa sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 imezipa mamlaka hizo suala zima la upangaji wa miji wakati halmahsuri hizo zina kazi nyingi na kujikuta zikizidiwa na kushindwa kupanga miji.

Pia sheria ya mwaka 1982 ina tamaka wazi kwamba serikali inauwezo wa kuchukua ardhi lakini wananchi kutolipwa fidia hilo pia ni tatizo.

Serikali iangalie ni namna gani itamaliza migogoro ya ardhi, sera za uwekezaji zifanyiwe marekebisho kwa mujibu wa sheria na taratibu juu ya ulipaji wa fidia.

Fidia haziendani na gharama za wakati ujao, wawekezaji wananufaika. serikali zisimamie sio kuachia halmashauri, serikali ina wataalamu wengi wa ardhi lakini haitambui umuhimu wa ardhi.

Maofisa wa aardhi waache kufanyakazi mezani pasipo kwenda kuangalia eneo husika pale wanapoombwa vibari  vya maeneo na wanananchi ndio maana wengi wanauza maeneo.

Muda wa umilikishwaji wa ardhi kwa wawekezaji upunguzwe na kuwa miaka 10 badala ya miaka 99 iliyoelekezwa kwenye sheria, serikali pia ina udhaifu katika kusimamia utawala wa sheria.

Kasi ya upimaji wa ardhi iongezwe ili kupunguza wimbi la watu kuvamia maeneo pasipo viongozi wa vijiji kujua na serikali za vijiji zipewe madaraka juu ya usimamizi wa ardhi.

Yatengwe maeneo makubwa ya wafugaji na wakulima pamoja na kuwawekea sheria zitakazowazuia wao kuingiliana kwa kuogopa sheria, ziwepo sheria za kumdhibiti mmiliki wa ardhi.

Pia wawekezaji watengewe maeneo yao si lazima wawe sehemu ambazo watu tayari wanaishi pamoja na wananchi kushirikishwa katika utaratibu wa ugawaji wa viwanja kwa kuwa ardhi ni maisha ya mtanzania.

No comments:

Post a Comment