19 January 2012

Madaktari kugoma

*Ni baada ya madai yao kutosikilizwa ndani ya saa 72
*Waliopo mikoani waagizwa kujiandaa na mgomo huo
 *Dkt. Nkya kuokoa 'jahazi' leo, serikali yapewa masharti

 Na Rehema Maigala

 CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimewataka wanachama wake wote nchini,
kujitaarisha kwa mgomo kuanzia leo kama mkutano wao na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Lucy Nkya, utashindwa kutoa suluhusho la madai yao.
Uamuzi huo umetolewa na madaktari hao walipokutana Dar es Salaam jana, baada ya muda waliotoa kwa serikali saa 72 kumalizika jana ili kushinikiza iwarudishe kazini madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wakati pande zote zikiafikiana kukutana leo, tayari zimeonesha kutoaminiana baada ya kutokea mvutano kila upande ukitaka kulipia ukumbi ambao watafanya mkutano huo.
Dhamira ya madaktari ni kulipia ukumbi ili waweze kushiriki mkutano huo kwa uhuru na kufikisha kero zao kwa Serikali.
Hofu ya madaktari kukataa Serikali isilipe ukumbi ni wao kuonekana waalikwa na muda wa mazungumzo kuwa mfupi.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika mkutano waliofanya jana, Rais ais wa MAT, Dkt. Namana Mkopi, alisema jana walikuwa wakutane na kutoa msimamo wao kwa Serikali lakini baada ya kutafakari kwa kina, waliamua kutuma ujumbe wizarani ili Waziri aweze kukaa nao meza moja na kusikiliza kilio chao.
Alisema baada ya ujumbe huo kwenda wizarani, ulirudi na taarifa kuwa Dkt. Nkya atafika baada ya saa moja kusikiliza kilio chao.
Baada ya muda huu kumalizika, Dkt. Nkya alipiga simu na kutueleza hatafika katika mkutano kwa sababu hakuwa na majibu ya maadi yetu hivyo alishauri tukutane leo mchana,¡± alisema.
Aliongeza kuwa, Dkt. Nkya alishauri madaktari hao watume wawakilishi 30 kwa ajili ya kufikisha kilio chao, pendekezo ambalo lilipingwa kwa madai kuwa, kila daktari ana hoja zake.
Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, madaktari hao wameibua madai mapya ambayo hayakuwemo wakati wanaipa Serikali saa 72.
Madai hayo ni pamoja na kutaka waongezewe posho, wapatiwe nyumba za kuishi na mengine yataibuliwa katika kikao hicho.
Dkt. Mkalisema licha ya madai hayo, pia wanataka kuona wagonjwa wanaowatibiwa wapo katika mazingira mazuri kwenye hospitali tofauti na sasa kwani wengine wanatumia kitanda kimoja kulala wagonjwa wawili au sakafuni ambako hakuna godoro.
Tunataka kufikisha ujumbe kwa Serikali ifaahamu kuwa kuanzia sasa, hatutatibu wagonjwa kwa kupewa vimemo na maofisa wa Wizara kwa saababu wagonjwa wote wana haki sawa ya kupata huduma inayofanana,alisema.
Aliongeza kuwa, pia hawatakubali kusaini barua ya kuridhia mbunge au kiongozi yeyote wa Serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi kama ugonjwa huo unawezekana kutibiwa nchini.
Hii inasababisha madaktari wa Tanzania tudhalaulika ndiyo maana hadi leo badala ya kwenda kuwatibia Watanzania tupo hapa tumejazana tunajadili kitu kinachosababishwa na watu wachache,alisema.

2 comments:

  1. Mwanzo mzuri kuna mambo mengi uozo katika sekta ya afya ambao madaktar wamefumbia macho, katka hali ya kawaida kwann mwanasiasa afanye check up nje ya nch kama mazngira ya ya hospita zetu wanajisfu wameboresha. Ningependa wananchi wafahamu n fedhaza wananchi znazotumikana mwanasiasa huyo haend peke yake
    Mgonjwa anatumwa toka nzega kuja muhimbili kwa kufanya vpmo kama CT SCAN, MRI au vp
    Mo vya damu katka hosptali ambayo mwez na zaid hakuna huduma hzo kwa sababu nyingne za kuskitisha eti hakuna chupa za kuchukulia damu,hakuna film za xray, hakuna dawa kwa ajil ya ct scan na hakuna dripu kwa dawa. Sasa huduma ya afya imegeuka siasa anapumbazwa nan? Tunasikitika hiz ajali znazotokea kila siku kuna mtu anajua ni wagonjwa wangap wanapotezamaisha kila dakika kwasababu ya uzembe wa watu? Tunaenda wap sasa cancer ya sisa imeingia had kwenye maisha ya watu

    ReplyDelete
  2. Ningependa kurekebisha kilichoandkwa kwenye hii taharifa. Siku ya juz madaktar tulikutana kuangalia siluhu ya mgogoro kwakuwa haikuwa busara kutafuta mshindi wakat afya za wanachi zkiwa hatarin hvyo tuliazmia kuonana naa wzara na naibu wazr alkubal kuja lakin aligundua hana majibu aliomba kukutana nasi lakin technicaly mkutano ni MAT wameomba meeting na ukumbi ungeamuliwa na mat hata hivyo wizara iliomba kusaidiana had kesho inafka wizara haikuwa na ukumbi MAT wakatafuta wakiwa tumeshatafuta ukumbi nibu anateua ukumbi wake saa sita akapewa taharifa kuwa madaktar wameshakutana. Hvyo aje chakushangaza baada ya masaa mawil akasema yeye anatangulia mnaz mmoja na anatoa nusu madaktar wamfuate la sivyo anaondoka.
    Kwanza nalaan kitendo cha naibu wazir kuonesha dharau ya waz na kuonesha nia yao ya kutotaka suluhu nan anaumia katka huu mgogoro

    ReplyDelete