19 December 2011

Kafulila kaponzwa na ubishi -Mbunge

*Asema amemshauri mara nyingi lakini hakusikia
*Afananisha tukio hilo la kihistoria na 'sikio la kufa'
*NCCR: kumpoteza mbunge gharama, hatuna jinsi
*Kafulila: Nilitokwa machozi kuwakumbuka wananchi

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, NCCR Mageuzi, Bw. David Kafulila, akiingia ndani ya gari lake, kwa ajili ya kuondoka Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana, baada ya kuvuliwa Uanachama.
 Na Rehema Mohamed

SIKU moja baada ya kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kumfukuza uanachama Mbunge wa
Kigoma Kusini Bw. David Kafulila, Mbunge wa chama hicho Jimbo la Kasulu Mjini Bw. Moses Machali, ametetea uamuzi huo kuwa ni sahihi.

Bw. Machali aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na chama hicho ili kutoa taarifa juu ya uamuzi uliofikiwa katika kikao hicho.

Alisema uamuzi wa kumfukuza Bw. Kafulila ndani ya chama hicho pamoja na wenzake ni sahihi akifananisha uamuzi huo na msemo wa wahenga kuwa 'sikio la kufa halisikii dawa'.

“Kafulila ni rafiki yangu mkubwa, nimewahi kumsihi mara nyingi kuhusu mwenendo wake lakini hakutaka kunisikia, kutokana na hali hii, itabidi anisamehe maana mimi huwa sipendi tabia za kinafiki.


“Wiki hii (iliyopita) kati ya Jumanne au Jumatano, Kafulila alionekana katika baadhi ya vyombo vya habari ambavyo ni TBC1 na ITV akisema chama hiki kinatekeleza matakwa ya chama tawala CCM, kimsingi hata mimi nimechukukia,” alisema.

Alisema matamshi hayo ni kashfa kubwa kwa chama hicho na yeye binafsi kama Bw.Machali.

“Inaniuma sana kumpoteza mbunge mwenzangu Bw. Kafulila lakini sina jinsi, huu ni utaratibu ambao umefuatwa kama zilivyo taratibu nyingine,” alisema Bw. Machali.

Aliongeza kuwa, Bw. Kafulila kama ataona ameonewa, anaweza kukata rufaa katika Kamati Kuu ya chama hicho au ngazi nyingine zinazostahili.

Alisema kosa alilofanya Bw. Kafulila ni kuzungumza mambo ya chama kinyume na utaratibu tena katika vyombo vya habari na yeye mwenyewe kukiri kutenda kosa hilo baada ya kuhojiwa na NEC.

“Kafulila alikiri kumchafua Mwenyekiti wa Taifa, Bw. James Mbatia, chama chetu kimefikia hatua hii kutokana na baadhi ya watu kutofuata kanuni na taratibu zilizowekwa,” alisema.

Wengine waliofukuzwa katika chama hicho ni Bw. Hashim Rungwe, ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia chama hicho, Kamishna wa chama hicho Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Bw. Mbwana Hassan na Bw. Yothamu Lubungira ambaye alikuwa Kamisha wa chama hicho Mkoa wa Tabora.

Akizungumzia uwamuzi huo, Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Bw. Samuel Ruhuza, alisema uamuzi huo unamfanya Bw. Kafulila kukosa sifa ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho.

Alisema chama hicho kimechelewa kuchukua uwamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa ni kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na Bw. Kafulila na kumshauri abadilike lakini haikuwezekana.

“Chama chochote cha siasa siasa kinafuata kanuni na taratibu walizojiwekea, hakuna mmiliki wa chama, hakuna bifu kati ya Mwenyekiti wetu Bw. Mbatia na Bw. Kafulila, kumpoteza mbunge mmoja kati ya wanne ni majonzi sana, ni sawa na kukatwa mkono au mguu.

“Kumpoteza mbunge ni gharama kwetu kwa sababu tutaingia katika uchaguzi mdogo, najua itakuwa majonzi kwa wenzetu wa Kigoma Kusini lakini tunaomba wasikwazike, tumelifanya hili kwa nia njema kabisa,” alisema Bw. Ruhuza.

Aliongeza kuwa, Bw. Kafulila na wenzake wana siku 14 za kukata rufaa kupinga uamuzi huo kama watahitaji kufanya hivyo.

Bw. Ruhuza alisema, hatua inayofuata sasa ni chama hicho kuwaandikia barua rasmi ya kuwavua uanachama na kupeleka taarifa rasmi katika mamlaka husika na kazi hiyo itafanyika leo.

Kwa upande wake akizungumzia uamuzi huo, Bw. Kafulila alisema sababu kubwa iliyomfanya atokwe machozi katika kikao cha NEC ni baada ya kuwakumbuka wananchi wa jimbo lake.

“Nimefanya mengi na nina mipango mingi ya kuwasaidia wananchi wa Kigoma katika nyanja mbalimbali, ufumbuzi wa tatizo hili utapatikana kwa njia ya mazungumzo au sheria za nchi,” alisema Bw. Kafulila.

25 comments:

  1. Mtamlaumu bure Kafulila ndg zangu yeye siyo kosa lake.Nadhani hiyo ni asili yetu ss watu wa Kigoma huwa tunabisha karibu kila kitu.Nadhani tuko "OBJECTIVE"

    ReplyDelete
  2. NCCR hebu msameheni huyo kijana kwani kilio chake kinaonyesha majuto. Kosa lake kubwa hapo naona ni kutoa siri za Chama kwenye vyombo vya habari. Kafulila ana mazuri mengi kuliko mabaya. Ni mtu muhimu sana hasa kwa mageuzi ya kidemokrasia tunayotaka katika nchi hii

    ReplyDelete
  3. jamani nccr tafadhali tumieni busara mrudisheni kafulila amefanya mazuri mengi saaana katika ujenzi wa demokrasia,chuki katika siasa hazifai,tulianza kuipenda nccr kwasababu ya kafulila na msimamo wake,kosa kama hilo linasameheka kulingana na nafasi aliyonayo kafulila,ana watu wengi wanamfuata,tafadhali waoneeni huruma wananchi wa kigoma kusini.

    ReplyDelete
  4. chondechonde nccr tafadhali mrudisheni kafulila.

    ReplyDelete
  5. Huyu jamaa kigeugeu, pepo lililomtoa chadema ndilo pia linamtoa nccr. Pole mbunge.

    ReplyDelete
  6. Kafulila ni makapi ya chadema. Tulijua kuwa hata huko nccr atavuruga tu. ni kijana mchochezi na anapenda kuwapindua wakubwa wake. hadema alikosana na dr slaa na mbowe ndo maana akatemwa.

    ReplyDelete
  7. Vijana lazima kujifunza kwa mbunge Kafulila,kwamba umaarufu hujengwa taratibu na kwa Tanzania kwa sheria iliopo umaarufu ni lazima uendane na chama chako!Mambo mengi yatabadilika kama tutapata katiba mpya inaotokana na wananchi!Lakini kwa bunge hili la posho, sina hakika kama katiba itapatikana.Rais amefanya kazi ya kikatiba ya kuweka sahihi, huu muda wa kupokea maoni unatoka wapi?Tanzania tuna shida!

    ReplyDelete
  8. kafurira hiyo ndiyo politiki ya Tz leo unakuwa popula kesho watu wanakusahau.

    ReplyDelete
  9. HAKA KAKIJANA KWAKWELI KAPU MBAFU SANA TENA KANA NYOODO KAMA KADEMU ISITOSHE KANAKAUJEURI FULANI BILASHAKA KAMETOKA NAO CDM, UNAKUMBUKA KALISHAWAHI KUFUKUZWA HUKO? SASA HUKU HAKAWEZI KUKA, SASA NDIYO KATAFUTE BIASHARA YA KUFANYA KATAWEZA KWAKUWA HUKO KUKIGOMA KATAENDA HATA MANYOVU KULETA BIDHAA ZA URUNDI. KWELI KAFULILA UMEFULIA KAMA KAJINA KAKO; KWAHERI BWANA MDOGO UMEZIDI KUROPOKA SASA............

    ReplyDelete
  10. nilijua tu, lazima wakumwage, Ubishi mpaka matakooni unaroho mbaya sana wewe Bwana mdogo ndiyo maana haunenepi; sasa uliyoyataka ndiyo haya na domo lako chafu kama ..... sawasawa NCCR Mageuzi kuvua gamba ndiyo kama huko mfano mzuri:

    ReplyDelete
  11. Kafulila pole sana,bishanga abashaija,mimi nakuhurumia haswa kwenye huo mkopo wa milioni 70 wa gari,utaulipaje na wewe umetoka prematurely.angalia usije ukafilisiwa wakajakuigiza wakina Commedy,kama kuna namna ya kuwapigia magoti viongozi wako fanya hivyo,utakuwa umejirudi,kosa ni kurudia kosa.Tunapenda jinsi unavyojenga hoja bungeni,it is too early to lose you,gone too soon..

    ReplyDelete
  12. Pole sana Braza K!!!! Ndo siasa ilivyo.

    ReplyDelete
  13. Kila Binadamu ana mapungufu yake.Biblia inasema samehe saba mara sabini. Hivyo naomba NCCR muhurumieni Ndugu yenu Kafulila

    ReplyDelete
  14. Ndugu yangu ya kaisali mpe kaisali na ya Mungu mpe Mungu.
    Kafulila anatakiwa atengeneze kwanza npo apate msamaha na kama inavyosemekana ameshauriwa mara nyingi sana.
    Jamani Sisi watu wa Kigoma huwa hatusikii mpaka kitokee ndipo tustuke (SISI NI WABISHI SANA HILI HALINA UBISHI TUNATAKIWA TUBADILIKE WANA KIGOMA LA SIVYO SIASA ITATUSHINDA)


    Elias

    ReplyDelete
  15. Hiyo ni kweli kabisa Kafulila.
    Kafulila fanya haraka wa kuombewa una tatizo si bure,Haiwezekani kila mahali wewe wakuonee tu. CCM, shida,CDM shida,NCCR shida sasa ndio maana ulikuwa unalia maana kila chama watakukataa na neema sasa inakukimbia,Hilo gari ulilikopeshwa na seriks=ali inawezekana bado hujamaliza kulilipa sasa itakuwaje na ndio maana ulilia sana, na si kweli kama ulikuwa unawalilia wapiga kura wako sio kweli ungekuwa hivyo usingekuwa na ubishi wa kushauriwa mara zote hizo na wala hukujali ,sasa ufukuzwe chama ndio ukumbuke wapiga kura wako ?usitudab=nganye bwana.Kiza kinene kilitanda ndio maana ulilia Lakini pole jipe moyo bado ni kijana utafanikiwa tu Lakini muhuuuuuuuuuu kazi.

    ReplyDelete
  16. WATANZANIA TUNAJIFUNZA NINI MATATIZO YANAYOTOKEA CUF NA NCCR? 1. CCM BADO INA NGUVU 2.VIONGOZI WETU HAWAKO TAYARI KUPINGWA 3.TUANGALIE UPYA SHERIA CHAMA KUWA JUU YA WANANCHI 4. CUF NA NCCR NI MAMULUKI WA CCM 5. 2015 TUINGUSHE CCM KAMA TUNATAKA AMANI HATA TUKIWEKA JIWE NI BORA

    ReplyDelete
  17. Kaa chonjo!!! Vyama vya upinzani vinaweza na vinathubutu kuvua gamba....Siyo kama wale walioanzisha dhana ya gamba - hadi kesho wanaimba tuuuuu! Sasa huyu kijana .. anaonekana ana akili, ila busara sijui...hivyo nadhani atafaa sana kwa wale wasiothubutu kuvua gamba, kapige hodi - uta-retain jimbo ndani ya CCM!

    ReplyDelete
  18. FOR EVERY ACTION THERE IS AN EQUAL AND OPPOSITE REACTION, BRO K LIFE IS LIKE THAT. WHEN ONE DOOR IS CLOSED 100 OTHER ARE CLEARLY OPEN.

    ReplyDelete
  19. Kafulila, usibweteke. Kama wapiga kura wako Kigoma Kusini bado wanakuamini kaa chini na washauri wako wazuri mjiandae kuendelea kuwatumikia wananchi.
    1. Kwanza hakikisha sheria nzima inayosimamia uchaguzi mdogo unaielewa vizuri na masharti yake unayaandalia na kuyafanya vizuri.
    2. Nenda jimboni haraka, kajieleze vizuri kwa wapiga kura wako wakuelewe na waendelee kukuamini
    3. Tafuta chama, hata kama ni cha muda mfupi kukuwezesha kurudi bungeni. Vyama vipo tele, sio CCM wala NCCR/CHADEMA/CUF pekee.

    ReplyDelete
  20. YAMETIMIA,HUKO NDIKO KUJUA KWINGI KUNAVYOWAPONZA WABONGO,KILA KITU WAJUA ETIII EEE??? SASA BRAZA KAKA "KUFULIA" UMECHEZEA SHILINGI KWA TUNDU LA TOILET, POLITICS ZIMEKUSHINDA ITS BETTER IF YOU STAY OR PRACTICE AGRICULTURE SI NDO KWANZA MULIPROPOSE KILIMO KWANZA NYIE

    ReplyDelete
  21. Hivi haka kajijana kamesomea fani gani? Siasa siyo kazi ya kumwingizia mtu mkate kwa hiyo kaanze kufikiri namna ya kubuni hata biashara ya kusambaza dagaa wa Kigoma kule Dodoma. Si yule mama Kinda ameamua watalii wa Dodoma waenziwe na posho nono? Basi hapa kuna soko bro, waulize hata machangu.

    ReplyDelete
  22. Mmmh watu mna toa comment utafikiri hata darasa la saba hamjamaliza!Kafulila CHADEMA hajafukuzwa bali alihamia mwenyewe NCCR.Hivi mnajua huko kwenye NEC ya NCCR walizungumza nini? Je hivi kusoma magazeti najua sio hulka ya Kitanzania basi hata kusia hatusikii,Mr.Mbatia hafai kuwa kiongozi, huwez kosa ubunge alafu uongoze kundi kubwa la watu jamani someni alama za nyakati.Mbatia kamwogopa Kijana yupo moto na anakubalika sana ndio maaana kamuundia zengwe aondoke!.OK kafulila ni mbaya sasa na Huyo Hashim Rungwe tena aligombea urais eti leo wamemtema tena na uanachama kabisa,looo makubwa balaa hilo. Wanauruho wa madaraka!.

    ReplyDelete
  23. TUANZE KUFIKIRI UPYA KUHUSU GHARAMA ZA UCHAGUZI BILLIONI 25 ZITOKE KWA UCHAGUZI MPYA WAKATI MTU KACHAGULIWA KUWA MBUNGE NA WANACHAMA NA WASIOWANACHAMA.TUSIUTAFUTE UMASIKINI BALI TUPAMBANE NAO.CHAMA KIKIMTUPA CHINI MTU WAKE BASI ALIYE FUATA KIIDADI YA KURA ACHUKUE UBUNGE.HII ITASAIDIA UMAKINI WA CHAMA KATIKA MAAMUZI YAKE NA PIA KULETA NIDHAMU NA BUSARA KATIKA KUTUMIKIA WATU NA CHAMA UNACHOWASILISHA. HILI PIA LINATUPA ANGALIZO KWA MGOMBEA BINAFSI AKIFANYA MADUDU NANI NA VIPI ATAADIBISHWA! ?

    ReplyDelete
  24. HUYU DOGO KAFULILA ATAKUWA NA MATATIZO,CHADEMA WALIMTEMA,HATA MIAKA MIWILI NCCR HAIJAFIKA ANALETA UBISHI.UJUAJI KWENYE UKWELI HAUSAIDII.HONGERA NCCR KWA KUFANYA UAMUZI MGUMU.CCM INGEKUWA HIVYO MAFISADI...

    ReplyDelete
  25. yeye si msemaji wa chama nini kilimuwasha kuropoka anazikosa 200000 hivi hivi

    ReplyDelete