Na Godfrey Ismaely
RAIS Mstaafu wa Marekani, Bw. George Bush anatarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi nchi, ziara ambayo itakuwa ya siku tano
zikiwemo nchi za Zambia na Ethiopia kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na taarifa iliyotolewa na Kituo Maalum cha Kutolea Taarifa zake mjini Dallas,Texas nchini Marekani Novemba 20 mwaka huu.
Taarifa ambayo kwa mara nyingine iliwasilishwa jana nchini kupitia vyombo vya habari na ubalozi wa nchi hiyo huku ikieleza kwamba ziara hiyo mbali na kuambatana na mkewe pia itajikita katika kuangalia miradi mbalimbali inayotekelezwa na jinsi ya kuendelea kuwasaida Waafrika.
"Rais George Bush ametangaza kupitia kituo chake cha taarifa kwamba atafanya ziara yake na mkewe katika nchi za Tanzania, Zambia na Ethiopia kuanzia Desemba 1-5 mwaka huu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza kwamba safari hiyo ya rais mstaafu wa Marekani Afrika inalenga kuendelea kujitolea kwa watu wa Afrika kwa njia ya kazi ya mpango maalum unaoendesha na taasisi yake ya (GWBI)hususan sekta za afya.
Hata hivyo mbali na uhamasishaji pia taarifa hiyo ilieleza kwamba, Bw. Bush atawasilisha ujumbe maalum kwa kushirikiana na wadau wengine wanaojihusisha na mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali kama saratani chini ya usimamizi wa serikali ya Marekani.
Aidha,ziara hiyo Afrika inalenga kusisitiza umuhimu wa kupambana na magonjwa mbalimbali hususan UKimwi, malaria na magonjwa mengine.
"Na kusherehekea mafanikio ya kuridhisha yaliyofanywa katika muongo mmoja uliopita kukabiliana na changamoto za magonjwa, umaskini na usalama. Aidha, ziara yao hiyo itaangalia kwa upande wa uangalizi juu ya njia mpya ya kuzuia saratani kwa wanawake kupitia uhamasishaji na washirika wakubwa kama 'Pink Ribbon Red Ribbon," ilifafanua taarifa hiyo.
"Mwaka 2001, Rais Bush alitangaza dhamira yake ya kwanza katika utawala wake wa kupambana na kuenea kwa magonjwa yanayozuilika katika Afrika. Muongo mmoja baadaye, watu 4,700,000 walipokea msaada wa kupambana nayo kupitia mfuko wa PEPFAR na Global Funds hadi kufikisha jumla ya watu 6,600,000 katika nchi zinazoendelea kuokoa maisha wanaopatiwa dawa za Ukimwi," iliongeza taarifa hiyo
Hata hivyo, hiyo itakuwa ziara ya kwanza kuifanya bara la Afrika kwa muda baada ya kustaafu urais tofauti na ziara za mwaka 2003 na 2008 na mkewe kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2005, 2006 na 2007.
Anakuja kukagua migodi yake ya dhahabu.
ReplyDeleteMnafikili anawapenda na anapenda muendelee kuishi hana lolote anakuja kukagua miradi yake iliyoipata bila sgida kwetu sisi wajinga tusiojua matumizi,POLE YETU
ReplyDeletepole watanzania na waafrica kiujumla hana msaada zaidi ya ukaguzi wa mali zake
ReplyDeleteUranium ya namtumbo , na mradi wake wa Barrick etc
ReplyDeleteni kweli Tanzania inathaminiwa na Bwana Bush kiasi hicho au kitu anatafuta hapa kwetu.
ReplyDeleteToka lini simba akafanya urafiki na swala ili waendelee kuishi kwa amani na utulivu, pole yetu sisi Wadanganyika. Bush utuletee vyandarua vingine kwani vile vya mwanzo tunafugia vifaranga pia tunavitumia kama uzio wa bustani, usisahau baba,chondechonde.
ReplyDeletekaribu rais bush ,njoo uchukue MADINI yako na uende tunakupenda sna kwa kuendelea kutufanya kuwa masikini.Na tunawependa viongozi wetu pia kwa kuwakumbatia kwa nguvu zote karibu sana mr BUSH
ReplyDelete