Na Godfrey Ismaely
WAZIRI wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Ana Tibaijuka, ametangaza kihama dhidi ya viongozi wa Halmashauri zote zilizikopeshwa fedha kwa ajili ya
kupima viwanja na kushindwa kuzirejesha.
Mbali na hilo pia waziri Tibaijuka, awaagiza wote wanaoendeleza ufugaji mijini wajiandae kuondoa mifugo hiyo mara moja kwa kuwa sheria ya mipango miji namba nane ya mwaka 2007 inazuia shughuli hiyo mijini.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya siku ya makazi Duniani, Waziri Tibaijuka alisema hawezi kuendelea kukaa kimya huku shughuli zilizoainishwa kisheria na kuridhiwa na wabunge zikisimama kwa uzembe wa watendaji wachache.
"Ukimya wa muda mrefu unatufanya tushindwe kuyafikia malengo yetu, kuanzia leo na kuendelea Halmashauri zote ambazo zilikopeshwa fedha na Wizara ili kupima viwanja kwa ajili ya kuviuza ama kuvigawa kwa wananchi zisiporejesha madeni hayo zikae tayari, kihama kimekaribia na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watendaji," alisema Profesa Tibaijuka.
Alisema kushindwa kwa halmashauri hizo kurejesha fedha hizo kunachangia utegemezi nyingine ambazo zilikuwa zinategemea fedha hizo kushindwa kupima viwanja hivyo ubadhirifu na hata tabia za kujimilikisha viwanja visivyopimwa kuendelea kila siku.
"Haiwezekani Halmashauri kukopeshwa fedha ili kupimia viwanja na baada ya kupima na kuviuza kushindwa kurejesha fedha hizo, hapa tutakuwa tunachokozana kwa kuwa halmashauri zingine zitashindwa kuendesha zoezi.
Kilichobakia kwa mtu anayekuchokoza ni vyema ukamchukulia hatua za kisheria, toka mwaka 2008 Wizara ilizikopesha Halmashauri za Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni zaidi ya sh. bilioni 1.4 ili kupimia viwanja ili nalo tutalifanyia kazi," alisema Profes Tibaijuka.
Akizungumzia ufugaji mijini unaoendelea alisema sheria ya nchi hairuhusu kufanya hivyo badala yake kwa muda mrefu walivumilia lakini kutokana na ukuaji wa miji tayari wizara inataka ufugaji huo usitishwe mara moja.
"Sheria hairuhusu kufuga mifugo mijini badala yake kama mtu ana shauku ya kufuga kabla ya kihama kumpitia ni vyema akaelekeza jitihada hizo vijijini kwa kuwa mijini kilichobakia ni kusimamia upangaji wa mipango miji na kuisimamia.
Kama watu watalipuuzia tamko hili basi wasinilaumu wakati nikitekeleza kile kilichoainishwa katika sheria ili kuweka miji yetu iwe safi," alisisitiza.
Mda si mrefu kikwete atamuondoa wizarani.
ReplyDelete