20 September 2011

100 washikiliwa Polisi Dar

Ngaillo Ndatta na Agnes Mwaijega

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikiria zaidi ya watu 100 kwa makosa mbalimbali yakiwemo wizi, kukutwa na dawa za kulevya, noti bandia, pombe
haramu ya gongo na ujambazi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyoanza Agosti 30 mwaka huu hadi jana ili kupambana na vitendo vya uhalifu na kuliweka jiji katika hali ya usalama zaidi.

“Kukamatwa kwao kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya jamii na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha nchi inakuwa na amani, pia tumekamata dawa bandia za kilimo na mifugo zinazosambazwa na matapeli, umakini wa wananchi unahitajikia,” alisema.

Alisema jeshi hilo pia limewatia mbaroni watu watano wakijiandaa kufanya uharifu katika Ubalozi wa Iran, wakiwa na mitungi miwili ya gesi, funguo bandia 13 na bisibisi mbili,

Watuhumiwa hao ni Respius Daniel (32), mkazi wa Mbagala Kongowe, Mbaraka Katuli (33), mlinzi nyumbani kwa Balozi na mkazi wa Ukonga Kitunda, Joshua Liala (36) mpishi wa ubalozini  mkazi wa Mbagala, Kelvin Shemsanga (26) mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security mkazi wa Njia Panda ya Kigogo na Michael Michael (40 ), mkazi wa Tabata Kimanga.

No comments:

Post a Comment