Na Zahoro Mlanzi
SIKU moja baada ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuitaka Yanga ijieleze kuhusu malipo ya John Njoroge, klabu hiyo imesema inalishangaa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushindwa kuwasilisha FIFA kilichojili katika sakata hilo.
FIFA, juzi iliitaka timu hiyo kueleza makubaliano waliyofikia ya kumlipa mchezji huyo kutokana na kukatisha mkataba wake kiholela, bila ya kumlipa fedha zake sh. milioni nne.
Akizungumza na gazeti hili mjini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Llody Nchunga, alisema suala hilo walijua limekwisha kutokana na maamuzi yaliyofikiwa katika kikao cha Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji kulitupilia mbali baada ya Njoroge kushindwa kufika siku ya kikao.
"Mimi sielewi hili suala kurudi tena, wakati kamati husika ililitupilia mbali baada ya mhusika (Njoroge) kushindwa kutokea siku ya kikao kutoa utetezi wake kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine waliokuwa wakitudai kwa wakati huo," alisema Nchunga.
Alisema pamoja na hilo, watawasilisha taarifa ya kile kilichojiri kama FIFA inavyotaka, lakini kikubwa watakachoeleza ni uamuzi uliofikiwa na kamati hiyo, ambapo kwa msingi huo ndio maana walikaa kimya.
Alisema kiutaratibu, Njoroge amefanya makosa kwenda moja kwa moja FIFA kwani kama asingeridhika na uamuzi uliotolewa na kamati hiyo, angekwenda mbele zaidi kwa kuwasilisha malalamiko yake katika Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo.
Alisema kama uamuzi ambao ungepatikana hapo, pia usingemridhisha, basi angekata rufani katika Kamati ya Rufani ya shirikisho hilo na baadaye ndio kupiga hodi FIFA, hivyo FIFA nao kulishughulikia hilo bila kufuata utaratibu waliouweka wenyewe, anapata hofu katika hilo.
Wachezaji wengine waliokuwa wakiidai Yanga ni Wisdom Ndhlovu, Steven Marashi, Ally Msingwa, ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakiidai sh. milioni 253.
Safi sana Njoroge,Kama hamjamlipa pesa zake mnasemaje eti mlijua hilo suala limeshakwisha.Hili ni tatizo kubwa sana kwa hizi timu mbili Simba na Yanga tena kwa upande mwingine hizi timu zinachangia sana kuharibu vipaji vya wachezaji.Sasa subiri mwakani tena uone watasajili wachezaji wangapi na kuacha wangapi.Kazi yao wazoea kucheza mpira mdomoni na kwenye magazeti.Mpira unachezwa uwanjani tena kwa vitendo na sio maneno.Oh tutaanika bunduki zetu,mkiingia uwanjani hakuna lolote.
ReplyDelete