05 August 2011

Eto'o aomba kuhamia mia Man City

ROME, Italia

MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o  ameitaka klabu ya Inter Milan  kuangalia kama Manchester City,  kweli inahitaji kumsaini baada ya kukorofishana na kocha wa timu hiyo, Gian Piero Gasperini.


Kocha wa City, Roberto Mancini,  anamhusudu sana Eto'o mwenye umri wa miaka 30, lakini nyota huyo wa Cameroon kama atakwenda City, atakuwa na changamoto ya kugombea namba.

Inter inamhitaji Carlos Tevez na hilo linaleta uwezekano wa timu hizo kubadilishana wachezaji, lakini City inampa thamani kubwa Tevez.

City pia inatarajia kuamua kuhusu hatima ya Emmanuel Adebayor katika siku chache zijazo, huku mwenyewe akitaka kusainiwa Real Madrid.

Wakati huohuo, beki wa kushoto wa City, Ryan McGi mwenye miaka 21, anajiunga na Crystal Palace kwa mkopo wa muda mfupi.

Mlinzi wa Stoke, Andrew Davies naye anajiunga na mkopo katika klabu ya Palace.

1 comment:

  1. lakini etoo kwa nini akorofishane na kocha au ni mbinu ya kuondoka inter baada ya timu hiyo kutofanya vizur kws sasa?

    ReplyDelete