19 July 2011

...Msuya atupa mzigo kwa Mkapa

*Asema ndiye ametufikisha tulipo

Na Godfrey Ismaely

MAKAMU wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya awamu ya Kwanza Bw. Cleopa Msuya ameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kutosha juu ya viongozi
wanaovuliwa au kujivua gamba wenyewe ili wakibainika kwamba walijipatia mali walizonazo kinyume na taratibu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Mwito huo aliutoa jana nyumbani kwake Dar es Salaam, wakati akifanya mahojiano maalum na Majira lengo likiwa ni kufahamu hatima na mwelekeo wa Taifa na tathimini yake juu ya mwenendo wa mambo ya siasa likiwamo suala la upatikanaji wa nishati ya umeme ambalo kwa sasa limeonekana kuwa kero kwa uchumi na hata uzalishaji.

"Lazima kila mmoja awajibike katika kutoa ufafanuzi awe amevuliwa au amejivua gamba mwenyewe kwa kuwa sisi wananchi tunachoitaji zaidi ni kuona hatua za kisheria zinachukuliwa dhidhi yao na ikiwezekana wawajibishwe," alisema Bw. Msuya na kuongeza.

"Zingatia kuna hatua za aina mbili ambazo zinaweza kuzaa matunda kwanza ni juu ya Chama kuwachukulia hatua za kuwapima watendaji wake na hata viongozi wanaotuhumiwa na vitendo vya ubadirifu kwa kuwavua wote madarakani.Hatua ya pili ni serikali kupitia vyombo vya dola hasa mahakama inapaswa kutumia vigezo vyake kwa kuzingatia kuwawajibisha wahusika na katika ili tunapaswa kuwa na 'Zero tolerance wakati wa kuwachukulia hatua'," aliongeza

Pia alisema kuwa suala la kuwafumbia macho viongozi wabadirifu madarakani ndiyo chanzo kinachochangia baadhi ya mipango ya maendeleo ya wananchi kutofanikiwa mapema.

"Ukienda katika Halmashauri utagundua kuwa hali ni mbaya kweli kutokana na watendaji ambao  wanajihusisha na suala la hongo hasa katika mpango wa kilimo kwanza katika hatua za kuagiza na kuwapatia wakulima powertiller hivyo hali kama hii haipaswi kufumbiwa macho bali hatua zinapaswa kuchukuliwa dhidhi yao mara baada ya uchunguzi," alisema Bw. Msuya.

"Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani siyo kwa dhumuni la kuwatumikia wananchi kama awali bali kujilimbikizia mali na hata kutekeleza mipango yao.Tuchukue mfano kwa Mwalimu, watoto wake na Mzee Kawawa utagundua kuwa licha ya kukaa madarakani kwa muda mrefu maisha yao ni ya kwaida kama watanzania wengine tofauti na sasa tunavyoshuhudia watu wameenda kujilimbikizia mabilioni nje ya nchi huku wakiyaita vijisenti, wengine wakijenga majengo na kuendesha magari ya thamani kubwa bila kujali maslahi ya wananchi," alisema Bw. Msuya.

UMEME

Bw. Msuya alisema kuwa suala la umeme hata kama litaendelea kupigiwa kelele kwa namna gani nchini kama serikali na hata vyama vya upinzani havitakaa kwa pamoja wakiwemo wataalam ili kuandaa michanganuo inayoeleza namna ya kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini zitakuwa kelele ambazo hazina tija.

"Hata misimamo iwekwe ya namna gani ya kutaka kuwashinikiza vingozi walioko madarakani wakiwamo wale wa Wizara ya Nishati na Madini wajiuzulu, ufumbuzi juu ya tatizo la kudhibiti mgawo wa umeme hauwezi kupatikana kwa kuwa kinachoitajika kwa sasa ni uwekezaji na michanganuo inayoonesha namna ambavyo rasilimali zilizopo hapa nchini kama makaa ya mawe, gesi,upepo na nishati ya jua inavyoweza kutumika kuzalisha umeme," alisema Bw. Msuya.

Alisema imefikia hatua kwa serikali kuwekeza zaidi katika nishati ya umeme kupitia mipango ambayo walikuwa wanatumia awali ya miaka mitano kwa madai kwamba rasilimali zilizopo hapa nchini zinaweza kuzalisha umeme wa kutosheleza kwa matumizi ya ndani na hata kwa ajili ya kuuza nje.

"Tatizo hili tunaloshuhudia la nishati linatokana na utaratibu usioridhisha katika serikali ya awamu ya tatu, kwa kuwekeza fedha vibaya na wala siyo awamu ya nne hawa walibebeshwa mzigo tu' kutoka kwa EPA, RICHMOND lakini  kwa mtazamo wangu ninaona waliohusika wote wakati wakiendelea kuchukuliwa hatua za kisheria serikali inaweza kuajiri na hata kuwatumia wataalam wa ndani na nje ili kuandaa michanganuo ya kutuondoa hapa tulipo sasa," alisema Bw. Msuya.


MALUMBANO BUNGENI

Bw. Msuya alisema kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani kwa sasa siyo kwa lengo la kuwasiadia ama kutatua kero za wananchi bali wamelenga maslahi binafsi.

"Ninakiri hadi leo hapa tangu 1992 mara baada ya serikali kufikia uamuzi wa kujiunga na mfumo wa vyama vingi sijamuona kiongozi mwenye uthabiti na mwelekeo wa kumsaidia mwananchi na hata kelele wanazopiga bungeni kwa sasa wala hazilengi kumsaidia mwananchi bali wanalenga maslahi yao tu.Kiongozi mwenye nia ya dhati kwa ajili ya kumsaidia mwananchi huwa anaadaa mchangunuo mzuri unaoelekeza jinsi ya kuzikabili kero za  wananchi wala siyo kusema tu,"alisema Bw. Msuya.

UCHUMI

Kwa upande wa uchumi alisema kuwa uwezekano wa Tanzania kuipita Kenya katika ukuaji wa uchumi wake kupitia kipimo cha GDP upo wazi kwa kuwa hali ilivyo kwa sasa mwelekeo huo upo ila kinachoitajika ni jitihada na uwajibikali kwa kila mtendaji na wananchi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hasa madini, vivutio vya ukalii, mbuga, gesi na mito.

"Uchumi wetu umeendelea kukua siku hadi siku kwa asilimia saba hadi kumi tofauti na Kenya ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia tatu hadi tano lakini kwa kupiga hatua zaidi. Tatizo ni kwamba ukuaji huo wala hauonekani kutokana na kutotumia vyema rasilimali zetu lakini ninaamini zikitumika vyema siku si nyingi tutaipita hata Kenya kiuchumi," alisema Bw. Msuya.

8 comments:

  1. Idiot! what he did during his tenure?

    ReplyDelete
  2. Huyu Kenge katoka mtoni sasa, hajui naye alikuwa kama wao, sasa anawacheka kwa sababu aling'atuliwa madarakani bila yeye kupenda. Hakumbuki aliwahi kuwaambia watanzania, kila mmoja abebe msalaba wake wakati akiwa waziri wa fedha. Ni kweli wahenga walisema, nyani anayemcheka mwenzake ahaoni kundule. Afadhali bwana Msuya utulie ule ulichojaliwa na walala hoi Watanzania.

    ReplyDelete
  3. Sema usichelee mabaradhuli waliofilisika kiitikadi wala kiimaadili NCHI IMEUZWA HII mipango mizuri muliyotuachia imevurugwa na hawa na hawa mafisadi waliyojiwekea hata mitandao ya kuwabeza wanao wakosoa! SIKU ZINAKUJA MTASEMA KILICHO MFANYA KUKU ASINYONYESHE. "Kila mtu kubeba mzigo wake!!" ni ukweli usiopingika na upo, ulikuwepo na unaendelea. Waliozoea kudanganywa unawekara. SUBIRINI MUBEBEWE MIZIGO NA NYIE MUPETE WANANGU!!!!

    ReplyDelete
  4. Sure, something must be done; Tanzania had something to be proud of .... but now The President is alone, of course he made some mistake somewhere by putting a large number of friends in every corner of government ... few to check and balance is ok .....but despite his good intention and vision he has now pilots to jet it off ..... Mr Msuya being near the president you can always advice, can't you sir? It is not a matter every body blaming and raising fingers it is a matter of taking action before it is too late, isn't it? We miss your good brains, for sure.

    ReplyDelete
  5. JE VIONGOZI WAILIO LITUMIKIA TAIFA HILI HAPO AWALI KWA DAMU NA USAHA HAWANA JUKWAA LA KUISAIDIA SERIKALI HATA KWA MAONI? KULE URUSI KUNA JUKWAA LA WAZEE WENYE BUSARA HAPA WANANGATULIWA .... WANAFUKUZWA .... WANAPUUZWA HATA NA WAHUNI. DUNIA HII MATAJIRI HAWATAKWISHA NA WALALA HOI HAWATATOWEKA ILA TUNATAFUFA JINSI YA KUISHI PAMOJA HAPA DUNIANI BILA KUJALI TOFAUTI ZA KIPATO KIJINSIA KIELIMU N.K AHSANTE MSUYA KWA KUPAAZA SAUTI.

    ReplyDelete
  6. Waheshimiwa ( na siyo viongozi ) wote wa chama Tawala, waliopita na waliopo ni walaji tu. Msuya asijifanye kujua. Aliila sana hii nchi.Siku zake Msuya alikuwa na kiburi ungedhani Tanganyika ilikuwa ya baba yake.Nikikumbuka napata kichefuchefu. Sisi wa siku zake tunakumbuka madhambi yake yote. Wote wakae kimya. Wananchi tunajua la kufanya katika uchaguzi ujao. Chukueni Chenu Mapema ( CCM ) muda wenu umekwisha.

    ReplyDelete
  7. Mzee Msuya asitake kujisafisha. Kama ni mzalendo wa kweli akiwa kiongozi msatafu alishindwa nini kumshauri Rais wa wakati ule, na hata kupiga kelele kwenye vyombo vya habari. Kama ni kiongozi anayejali maslahi ya nchi, ebu atupe thamani ya mali ya umma anayotumia kama kiongozi mstaafu, thamani ya gari lake, gharama za matibabu anazodai kulipwa ?

    ReplyDelete