20 July 2011

Bajeti ya Ngeleja sasa Agosti 13

Na Gladness Mboma, Dodoma

BAADA ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kukwaa kisiki bungeni na serikali kuamua kuondoa hoja, sasa waziri wa wizara hiyo, Bw. William  Ngeleja, atasimama
bungeni kuwasilisha makadirio  makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake Agosti 13 mwaka huu.

Kwa mujibu wa marekebisho ya ratiba ilitolewa jana,  inaonesha kuwa wizara hiyo imepewa muda wa siku moja badala ya muda wa siku mbili uliokuwa awali.
 
Juzi wabunge walikataa kupitisha bajeti wa wizara hiyo kwa msimamo kuwa haioneshi suluhisho la tatizo la umeme nchini.
 
Baada ya Waziri Mkuu,Bw. Mizengo Pinda, kusoma upepo huo, aliamua kusimama bungeni na kutoa kauli ya kuondoa hoja na kuomba bajeti hiyo iwasilishwe upya baada ya wiki tatu.

No comments:

Post a Comment